Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DRFA yakabidhi kitita Yanga

Chama cha Mpira wa Miguu Dar es Salaam (DRFA) leo kimekabidhi kiasi cha Sh3 milioni kwa Yanga ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotoa mwishoni mwa wiki ya kutoa Sh1 milioni kwa kila bao ambalo litafungwa na Yanga na Simba kwenye mechi zao za mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Raja Casablanca na TP Mazembe.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo na mwenyekiti wa DRFA, Lameck Nyambaya kabla ya mchezo baina ya KMC na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na zimepokelewa na nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto.

Katika mchezo huo dhidi ya TP Mazembe, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuifanya isogee hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika.

Lakini wakati Yanga ikivuna fedha hizo, mambo hayakwenda vizuri kwa watani zao Simba ambao wameondoka patupu baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya Raja Casablanca kwa mabao 3-0.

Kabla ya DRFA kutoa ahadi hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitoa ahadi ya kutoa Sh 5 milioni kwa kila bao ambalo Simba na Yanga zingefunga kwenye mechi zao za hatua ya makundi.

Akizungumzia ahadi hiyo, mwenyekiti wa DRFA, Lameck Nyambaya alisema itakuwa na muendelezo.

"Huu ni mwanzo tu kwani lengo letu sisi DRFA ni kuona timu zetu zinafanya vizuri na kuzidi kuutangaza vyema mkoa wa Dar es Salaam."

"Ni imani yetu kwamba katika mechi zao zitakazofuata, Yanga na Simba zitafanya vizuri kwa kupata ushindi ugenini ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali," alisema Nyambaya.