Djibouti wanaitaka fainali CECAFA U-20
Muktasari:
- Kikosi hicho kilichowasili Tanzania juzi Jumamosi kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Septemba 15 hadi 25, 2026, huku viongozi wa Shirikisho la Soka la Djibouti wakisisitiza umuhimu wa vijana hao kupambana hadi kufikia malengo yaliyowekwa.
TIMU ya taifa ya Djibouti ya vijana chini ya miaka 20 imewasili Tanzania ikiwa na lengo la kucheza fainali ya michuano ya CECAFA U-20 itakayowapa tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20.
Kikosi hicho kilichowasili Tanzania juzi Jumamosi kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Septemba 15 hadi 25, 2026, huku viongozi wa Shirikisho la Soka la Djibouti wakisisitiza umuhimu wa vijana hao kupambana hadi kufikia malengo yaliyowekwa.
Wachezaji hao waliagwa katika kituo cha akademi ya soka na hafla hiyo kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Djibouti pamoja na viongozi wengine waandamizi wa soka na michezo, akiwemo mkurugenzi wa shirikisho, Hassan Ali na mkuu wa msafara wa timu hiyo ya U-20, Said Bouha.
Viongozi hao waliwataka wachezaji kuiwakilisha Djibouti kwa heshima na kucheza kwa kujituma katika kila mchezo watakaokutana nao kwenye michuano hiyo. Djibouti imepangwa Kundi B pamoja na Uganda na Sudan, huku michezo yote ya kundi hilo, kila mchezo utakuwa muhimu kwa Djibouti kwani makosa madogo inaweza kuwagharimu, hasa katika mechi za mwanzo ambazo zinaweza kuamua hatima ya timu hiyo.
Djibouti inawinda nafasi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika U-20, kwani timu mbili zitakazofika fainali ya michuano hii ndizo zitakazoiwakilisha CECAFA katika fainali hizo mwaka 2027 nchini Ghana.