Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Fei Toto lafikia pazuri, mchongo mzima upo hivi...

TOTO Pict


TAIFA Stars inatarajiwa kushuka uwanjani Jumapili hii kukabiliana na wenyeji Morocco katika mechi ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, mechi inayotajwa kuwa ndio ya kuamua dili la kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’.


Fei ndiye aliyeivusha Stars kutinga hatua hiyo ikiwa ni rekodi tangu Tanzania ilipoanza kushiriki michuano hiyo mwaka 1980, huku akiwa na dili linalosubiri amalize majukumu yake katika michuano hiyo ya AFCON ili asainiwe.


Ipo hivi. Baada ya kutulia kwa siku kadhaa, Fei Toto amerudi tena katika kutengeneza vichwa vya habari. Tena safari hii kwa kishindo kizito. Achana na ombi la Anko Nzala aliyemtaja bilionea na Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed ‘MO’ Dewji kumsajili kiungo mshambuliaji huyo, kuna Waarabu walioanza mazungumzo na Azam.

Kwa wanaokumbuka kipindi cha dirisha kubwa la usajili alihusishwa na Simba, Yanga, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, lakini kwa bahati Agosti klabu inayommiliki Azam ilitangaza kumuongeza mkataba hadi mwakani.

Hata hivyo, mwishoni mwa mwaka jana klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya ilijitokeza na sisi Mwanaspoti tuliripoti taarifa hiyo kuletwa kwa ofa ya Sh 4.5 bilioni na Waarabu hao ili wamsajili kupitia dirisha dogo lililofunguliwa.

FEI 01

Sasa taarifa ni kwamba matajiri hao wa Libya wamekuwa wakimfuatilia Fei kupitia mechi za Stars na kuridhishwa naye na kwamba wanasubiri kumalizika kwa michuano huyo (hasa kama Stars itaishia njiani mbele ya Morocco) ili kukamilisha dili hilo ambalo kwa sasa linaelezwa lipo zaidi kwa mchezaji baada ya klabu ya Azam kuridhia.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, Al Ahli Tripoli kupitia kwa mawakala wao, wakamtafuta binafsi kiongozi mmoja wa Azam FC na kuelezea nia yao na kujibiwa watume ofa ili klabu iipitie na kuona nini kitatokea.

Wakala akatuma ofa hiyo kupitia email yake binafsi kwa huyo kiongozi na kwa mchezaji mwenyewe na inaelezwa hilo lilikuwa kosa kubwa la kiufundi kumtumia ofa hiyo mchezaji na kuanza kusambaa kitu kilichoikera Azam FC na kutaka watume tena email kwa anwani ya klabu na sio mchezaji, ili mambo yawe mepesi.

FEI 02

Wakala akafikisha ujumbe kwa Al Ahli Tripoli na bila ajizi wakatuma ofa yao moja kwa moja kwenye anwani za Azam FC na ikafanywa tathmini ya kiufundi kuona kama waikubali au waikatae ofa hiyo ya Sh4.5 bilioni na ikaainisha wazi kwamba kama Fei atakubali ofa atapewa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya jumla ya zaidi ya Sh10 bilioni.

Hiyo ni thamani ya jumla, kwa maana ya pesa zake za kusainia mkataba na mshahara atakaolipwa katika wakati wake wote klabuni hapo pamoja na motisha nyingine kama bonasi, ikielezwa hiyo ilitumika awali kumshawishi nyota huyo avunje mkataba na Azam, jambo alilolikataa kuepuka yaliyotokea mwaka 2023 alipoondoka Yanga.


FEI 03

MCHONGO ULIVYO

Taarifa mpya ni kwamba kila kitu kimekaa vyema na kwamba mabosi wa Libya wanasubuiri mchezaji huyo atoke AFCON ili watue jijini Dar es Salaam kukamilisha dili hilo na kumbeba Fei Toto kupitia dirisha dogo.

“Kila kitu kimekaa vyema hadi sasa, Al Tripoli ilikuwa inasubiri kumalizika kwa AFCON au Stars itolewe mapema waje wamalizane na mabosi wa Azam kwani hata mchezaji ameshakunjua roho kwa ofa alizowekewa,” kilisema chanzo cha kuaminika kutoka Azam FC.

Awali, Fei alikuwa amepewa mechi mbili za awali za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Azam FC inashiriki ikiwa Kundi B sambamba na Wydad Casablanca ya Morocco, Nairobi United ya Kenya na AS Maniema ya DR Congo. Mechi hizo za awali zilikuwa ni dhidi y Maniema na Wydad ambazo zote Azam ilipasuka kwa mabao 2-0, lakini ghafla ikaja michuano ya AFCON Waraabu wakaona waitumie kumsoma vizuri nyota huyo.

Katika Afcon, Fei amecheza mechi mbili dhidi ya Uganda na Tunisia na amefyunga bao lililoipeleka Stars 16-Bora.

Bao lake limeivusha Stars kucheza hatua ya 16 Bora inayoanza kesho Jumamosi, japo yenyewe itacheza Jumapili dhidi ya wenyeji Morocco kuamua tuimu ya kwenda robo fainali.

Matokeo ya mechi hiyo ya keshokutwa, kama Tanzania itaishia hapo basi itaharakisha Waarabu kufanya biashara na Azam juu ya kiungo mshambuliaji huyo mwenye mabao mawili na asisti moja katika Ligi Kuu Bara iliyosimama tangu Desemba 7 ili kupisha fainali hizo za Morocco.