Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dante amgomea Ngoma Yanga

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Dante alisema Ngoma ni mshambuliaji mzuri ila kusepa kwake Yanga kwenda kutua Azam hakutaiathiri timu yao endapo mabosi wa Yanga watatafuta mshambuliaji mwenye makali zaidi ya Mzimbabwe huyo.

BEKI kitasa wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ anatambua mkataba wake na klabu hiyo upo ukingoni na hatafanya maamuzi ya haraka katika kukimbilia ofa anazopata. Pia amefunguka juu ya kuondoka kwa straika Donald Ngoma akisema aachwe aende zake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dante alisema Ngoma ni mshambuliaji mzuri ila kusepa kwake Yanga kwenda kutua Azam hakutaiathiri timu yao endapo mabosi wa Yanga watatafuta mshambuliaji mwenye makali zaidi ya Mzimbabwe huyo.

Dante aliyekosa mechi tatu za mwishoni mwa msimu uliofunga pazia jana Jumatatu kufuatia kuugua malaria, alisema anatambua endapo Ngoma atapona na kurejea uwanjani akili yake itataka kuifunga Yanga, lakini haoni kama kazi hiyo itakuwa rahisi kwake kwani wao wanajua wapi pa kumdhibiti.

“Uongozi unatakiwa kutafuta mshambuliaji wa maana zaidi ya Ngoma ili azibe nafasi yake. Akipatikana huyo hata tukutane na timu yenye washambuliaji gani kazi yetu mabeki tutaifanya vizuri na sioni kama walikosea kilichotokea kwa Ngoma kinaweza kunitokea hata mimi, timu haiwezi kusubiri kwa muda mrefu kukosa huduma yako na huku timu haifanyi vizuri,” alisisitiza beki huyo mkali wa mipira ya juu.