Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DABI YA KARIAKOO: Hoja mpya za wazee Yanga

WAZEE Pict
WAZEE Pict

Muktasari:

  • Wanachama hao waendelea kusisitiza kwa kusema; ‘HATUCHEZI’ huku wakitoa hoja mpya kwa mabosi wa klabu hiyo kama wanatakiuka msimamo huo, basi wajue mlango wa kutoka utakuwa wazi.

KAMA unadhani Yanga wanatania juu ya tishio lao la kuigomea Dabi ya Kariakoo iliyopangwa Juni 15 basi utakuwa umekosea, baada ya wanachama wa matawi wakiongozwa na wazee wa klabu hiyo kutoa msimamo mzito jana wakiupiga mkwara uongozi.

Wanachama hao waendelea kusisitiza kwa kusema; ‘HATUCHEZI’ huku wakitoa hoja mpya kwa mabosi wa klabu hiyo kama wanatakiuka msimamo huo, basi wajue mlango wa kutoka utakuwa wazi.

Ipo hivi. Hatma ya pambano hilo namba 184 la Ligi Kuu Bara ikiwa ni kiporo cha Dabi iliyoshindwa kuchezwa Machi 8, inazidi kuwa ngumu baada ya uongozi wa Matawi ya Yanga kutoa msimamo mkali ukiweka rehani mechi hiyo wakisema hawatacheka na yeyote.

Mkutano uliofanyika jana katika makao ya klabu hiyo, wanachama hao wa matawi wakijumuishwa wazee walitoa msimamo mkali kwa uongozi wa juu kuhusiana na mechi hiyo wakisema timu hiyo haitakwenda uwanjani hdi mambo yao ya msingi yafanyiwe kazi.

Wakizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mohammed Msumi alisema hadi sasa inapangwa tarehe ya mechi hiyo inayotakiwa kupigwa Juni 15, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wala Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) haujatoa sababu za msingi zilizosababisha mechi ya Machi 8 kuahirishwa.

“Kuna msimamo ambao uongozi wetu uliwaandikia Bodi na TFF, lakini hadi sasa hakuna majibu ya maana yaliyorudishwa, zile sababu ambazo ambazo walizitoa zilizoahirisha ule mchezo majibu yake ni yapi, tunakwendaje kucheza mechi hii wakati kuna maswali magumu nyuma?” Alisema Msumi.

Mratibu wa matawi hao ya Yanga, Shaaban Mgonja alienda mbali akisema mkutano wa matawi umekubaliana kwamba, hakutakuwa na mchezo huo na endapo kiongozi wao yeyote atakayeona anakwenda kinyume na msimamo huo anarubusiwa kupisha klabuni hapo kwa kuondoka.

“Viongozi wetu tunawaambia mlilianzisha, Yanga haitapeleka timu hili tumekubaliana na kama kuna kiongozi kuanzia Rais hadi wa chini kabisa anaona hakubaliani na hili mlango ule pale upo wazi aondoke,” alisema Mgonja, huku Edwin Kaisi amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutoka mikoani na kwingineko kutofanya maamuzi ya kukata tiketi kwa kuwa Yanga haiitambui mechi hiyo.

“Ndugu zetu mnaotoka mikoani na kwingineko msikate tiketi wala kuja uwanjani, msisafiri Yanga haitapeleka timu, wale ambao mnafanya biashara acheni kukopa pesa kwa maandalizi ya hii mechi mtapata hasara tumeona tuwajulishe mapema ili msiingie gharama zisizo na msingi,” alisema Kaisi.

“Kwanza hawa TFF na Bodi wanatakiwa kuwapa majibu ya viingilio vya mchezo wa kwanza vilikwenda wapi, wanaohusika kutangaza mechi hii tunawaomba waache kutumia logo la klabu kwa kuwa hatutashiriki hii mechi.”

Wakati Wananchi wakitoa msimamo huo, Bodi ya Ligi kupitia Ofisa Habari, Karim Boimanda alinukuliwa kwamba mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kwamba tayari za mchezo huo zinaendelea kama zilivyoanishiwa katia tangazo ya bodi ilipoupanga upya Juni 15.

Mechi hiyo ilikwama kupigwa Machi 8 kwa kilichoelezwa ilitokana na Yanga kudai kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo na kutishia kutocheza kabla ya Bodi ya Ligi kutangaza kuahirishwa kwa sababu ya hali ya kiusalama na kuwepo kwa mambo yanatohitaji uchunguzi wa kina.

Hata hivyo, hakuna taarifa nyingine iliyowahi kutolewa na Bodi ya Ligi juu ya uchunguzi ulioufanyika juu ya mechi hiyo ya awali na badala yake imesisitiza mechi itapigwa Juni 15 kwa viingilio vilevile vilivyolipwa kwa mchezo wa Machi 8, huku Yanga ikisisitiza kwamba haichezi na haina imani na bodi.

Kwa mujibu wa kanuni ya Ligi, timu isiyofika uwanjani kwa mechi moja inapoteza pointi tatu na mabao matatu, lakini itakatwa pointi 15 katika zile ilizonazo, jambo ambalo Yanga imekuwa ikisisitiza ipo tayari mradi, kwa maelezo Bodio ilishindwa kusimamia kanuni hizo za Ligi katika mechi ya Machi 8.

Hilo ni pambano la 114 kwa watani wa jadi kama watakutana Juni 15 katika mechi za Ligi tangu mwaka 1965 na pambano la kwanza msimu huu, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 86 na beki wa Simba, Kelvin Kijiri aliyejifunga wakati akiokoa shambulizi lililotokana na mpira wa Maxi Nzengeli.