Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cecafa yaipongeza Tanzania, Uganda, Burundi, Kenya kufuzu Afcon

Muktasari:

Hii ni mara ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwa na timu nne katika mashindano ya Afcon

Dar es Salaam. Baraza la Vyama Vya Michezo wa Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limezipongeza timu nne za ukanda wake kwa kufuzu fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) yaliyopangwa kufanyika nchini Misri mwezi Juni na Julai.

Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi zimefanikiwa kufuzu katika fainali hizo zilizopangwa kuanza Juni 21 mpaka Julai 19 mjini Cairo.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema kuwa kitendo cha kuingiza timu nyingi katika mashindano makubwa ya Mataifa ya Afrika ni ushahidi tosha kuwa soka la ukanda wa Cecafa linazidi kupata maendeleo makubwa na kuomba nchi ambazo hazijafikia hatua hiyo kujitahidi.

“Kwa kweli hii ni sifa kubwa kwa Cecafa na heshima kwa mchezo kwa ujumla. Ni miaka mingi hatujawahi kupata timu nyingi katika mashindano makubwa ya Afrika, kwa kweli in ni faraja kwetu,” alisema Musonye.

Musonye amesema kuwa ni wakati wa kuanza maandalizi ya fainali za Afcon ambazo ni mashindano magumu kutokana na kushirikisha timu magwiji ya soka ya bara la Afrika.