Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Casemiro: Yanga imenijenga kuwa imara

Muktasari:

  • Casemiro alisema kucheza katika mazingira ya ushindani akiwa Yanga kumemjengea kujiamini, jambo ambalo amelitumika alipovaa jezi ya Ngorongoro Heroes katika michuano ya CECAFA U-20.

KIUNGO wa Ngorongoro Heroes, Abdulnassir Mohamed 'Casemiro', amesema uzoefu alioupata ndani ya kikosi cha Yanga, umekuwa msaada mkubwa katika safari yake ya kwanza ya kucheza timu ya Taifa ya vijana.

Casemiro alisema kucheza katika mazingira ya ushindani akiwa Yanga kumemjengea kujiamini, jambo ambalo amelitumika alipovaa jezi ya Ngorongoro Heroes katika michuano ya CECAFA U-20.

“Uzoefu nilioupata Yanga umenisaidia sana, hasa kwenye suala la kujiamini na kucheza kwenye presha. Nimeweza kuutumia uzoefu huo hapa Ngorongoro,” amesema Casemiro.

Kiungo huyo amesema kucheza timu ya Taifa kumekuwa hatua muhimu kwake, hasa kwa kuwa ni  mara yake ya kwanza kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika ngazi hiyo.

“Kucheza timu ya Taifa ni kitu kikubwa kwangu. Nimejifunza vitu vingi na kila mchezo umekuwa ukinipa uzoefu zaidi,” amesema Casemiro.

Ngorongoro Heroes imefanya vizuri katika michuano hiyo na kufanikiwa kufika fainali baada ya kuichapa Burundi mabao 2-0 kwenye nusu fainali.

Ushindi huo umeiwezesha Tanzania kufuzu kwa mara ya pili mfululizo katika historia yake kwa fainali za AFCON U-20, ambazo zitafanyika Ghana mwaka 2027.

Casemiro amekuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho akitumika katika eneo la kiungo, akisaidia timu kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji pamoja na kusambaza mipira.

"Tuna furaha kwa kufuzu AFCON, lakini bado tuna kazi ya kumaliza mashindano haya vizuri, kila mmoja wetu anataka kuendelea kupambana hadi mwisho,” amesema Casemiro.

Ngorongoro Heroes sasa inaelekeza nguvu katika mchezo wa fainali dhidi ya Sudan utakaochezwa kesho Alhamisi, huku kikosi hicho kikilenga kumaliza mashindano kwa kutetea ubingwa wake.

Casemiro aliyetua Yanga Julai 2025 akitokea Mlandege ya Zanzibar, uzoefu huo alioupata unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya maendeleo yake katika soka.