Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Black Sailors shida iko hapa ZPL

SELER Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar, imeruhusu mabao manane na kufunga sita ikikusanya pointi nane sawa na ilizonazo Kipanga iliyopo nafasi ya nane.

TIMU ya Black Sailors imeeleza kuwa makosa ya ndani ya timu yamechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya KMKM, ambapo kocha wa timu hiyo, Ali Khamis Ali akiitaka safu ya ulinzi kufanyiwa maboresho kabla ya mchezo unaofuata.

Mabaharia hao weusi waliopanda daraja msimu huu watachuana na JKU, Oktoba 12, 2026 kwenye Uwanja wa Pangatupu uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kocha wa Black Sailors, Ali Khamis Ali, amesema timu hiyo ilishindwa kupata matokeo bora kutokana na makosa yaliyofanywa na wachezaji hususani katika safu ya ulinzi ikiwemo kuondoa mipira ya hatari kwa wakati.

Amesema baada ya kosa hilo timu ilikumbwa na changamoto nyingine ikiwemo kuonyeshwa kadi nyekundu, hali iliyowapa KMKM nafasi ya kuongeza shinikizo na kufunga bao la pili. 

Kocha huyo amesema pamoja na matokeo hayo, anashukuru kuwa wachezaji wote walimaliza mchezo wakiwa salama bila kupata majeraha makubwa. 

Akizungumzia safu yao ya ulinzi, kocha huyo alikiri kuwa bado kuna makosa ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi, katika mazoezi ili kuzuia timu kuendelea kuruhusu mabao ya aina hiyo.

“Tathmini ya jumla ya timu kwa sasa ni ya wastani kwani tumepanda daraja, hivyo inahitaji muda kujenga uzoefu,” amesema.

Amesema hali hiyo ni tofauti na KMKM ambayo ina uzoefu wa miaka mingi katika Ligi Kuu, hivyo kikosi chake kinaendelea kujifunza na kujenga uzoefu kadri msimu unavyoendelea. 

Timu hiyo ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar, imeruhusu mabao manane na kufunga sita ikikusanya pointi nane sawa na ilizonazo Kipanga iliyopo nafasi ya nane.