Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biashara kuwakosa wanne dhidi ya Mbeya Kwanza, Kocha awatoa wasiwasi

Kocha wa timu ya Biashara United, Vivier Bahati (kulia) akielezea maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya Kwanza utakaochezwa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Picha na Damian Masyenene

Muktasari:

  • Biashara United inakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ikivuna pointi 19 huku Mbeya Kwanza ikishika mkia na alama zao 14.

TIMU ya Biashara United ya Mara itaendelea kukosa huduma ya kiungo wake, Ramadhan Chombo 'Redondo' na wenzake watatu katika mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mbeya Kwanza kesho.

Mchezo huo utachezwa kesho Jumatano Aprili 6 kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo timu hizo zilizo mkiani mwa msimamo wa ligi zitaumana kusaka pointi za kuwasogeza juu huku kiingilio kikiwa Sh 3,000.

Chombo ambaye amekuwa mchezaji muhimu na mwandamizi ndani ya kikosi hicho hajaonekana katika mechi mbili za timu hiyo kutokana na majeraha ambapo Kocha Vivier Bahati amesema atakosekana tena kesho kutokana na sababu za kifamilia baada ya kupewa ruhusa ya kushughulikia mambo yake ya kifamilia.

Bahati amewataja wachezaji wengine watakaoukosa mchezo huo ni James Mwashinga ambaye ana kadi tatu za njano, Mpapi Nassibu na Aniceth Revocatus ambao wanasumbuliwa na majeraha mbalimbali waliyoyapata kwenye mechi za kirafiki jijini Mwanza.

Licha ya kuwakosa nyota hao, Mrundi huyo amewatoa wasiwasi mashabiki na kutamba kuwa kila mchezaji ni muhimu kikosini na mipango yao itakwenda kadri wanavyotarajia huku akikazia kuwa maandalizi waliyoyafanya yanatosha kuwapa alama tatu muhimu.

"Kukosekana kwa wachezaji hao wala siyo shida tuna kikosi kizuri kila mmoja ni muhimu kikosini, timu iko vizuri tumepata muda wa kutosha wa kupumzika na kujiandaa," ameesema na kuongeza

"Maandalizi yetu yalikuwa mazuri tulichokuwa tunakihitaji tumekuona, tumeona mapungufu yetu tumeyafanyia kazi bila shaka tutaona kwenye mchezo huo,"

Kipa wa timu hiyo, Daniel Mgore amesema wachezaji wanatambua nafasi iliyopo timu yao na wameapa kuipigania kwenye mechi zao zote ukiwemo wa kesho ili kupata ushindi.

"Wachezaji tumejiandaa vizuri tunajua umuhimu wa mchezo huu tukifuata maelekezo ya walimu tutafanya vizuri lazima tujitolee tuisaidie timu," amesema Mgore.