Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BERLIN YATEKWA: Jiji zima njano, nyekundu zatawala

Muktasari:

Jiji la Berlin lilikuwa katika mwonekano tofauti, maelfu ya mashabiki waliuteka mji, makao makuu ya nchi yakawa kama bahari yenye rangi ya njano ambayo unaweza kuitofautisha kidogo kwa kialama chekundu kilichochomoza

KATIKA toleo lililopita kwenye kitabu cha Pep Confidential, mwandishi Marti Perarnau alimalizia mazungumzo yake na Arjen Robben kwa kumuuliza kuhusu mfumo mpya wa Kocha Pep Guardiola na namna alivyoanza kuuzoea mfumo huo. Sasa endelea…
Perarnau: “Timu itakuwa bora zaidi kwa sababu umeanza kuuzoea mfumo mpya wa uchezaji?
Robben: “Haswa, mwaka wa kwanza chini ya kocha mpya mwenye staili mpya ulikuwa mgumu na mwaka huu tumeshinda mataji matatu, tumevunja rekodi ya Bundesliga, tumecheza nusu fainali ligi ya mabingwa na tunasubiri kubeba Kombe la Ujerumani. Hiyo ni rekodi ya kuvutia kwa mwaka wetu wa kwanza, na sisi wachezaji tunafahamu kwamba tunaweza kuwa bora zaidi mwakani kwa sababu tunaelewa kila kitu kwa ubora zaidi.
Ni mazoezi ya mwisho ya msimu jijini Berlin kwenye Uwanja wa Olympic na wakati David Alaba akiruka kuwania mpira wa juu akagongana na Ribery na kuumia tumboni. Kwa hiyo Alaba hakuwa na nafasi ya kucheza mechi ya fainali na Dortmund. Ni pigo kwa timu.
Baada ya chakula cha jioni, Pep alimwita Rafinha na kumuuliza, “Rafa unaweza kucheza upande wa kushoto? Jibu la Mbrazil huyu likawa wazi, “Pep unajua naweza kucheza eneo lolote utakaloniambia.”
Hiyo inamaanisha tayari Pep alikuwa na mbadala wa kucheza nafasi ya Alaba lakini hatua hiyo maana yake ni alilazimika kuchezesha mabeki wa pembeni wanaotanua uwanja kuliko alivyopanga awali na kilichobaki hapo ikawa ni kutafuta mtu wa kucheza nafasi ya Rafinha upande wa kulia lakini aliamua kufanya uteuzi huo akiwa amejituliza kitandani usiku akiusaka usingizi.
Jumamosi asubuhi mara tu baada ya kupata kifungua kinywa, akaanza kwa kumshirikisha Hojbjerg na habari zile, Hojbjerg alikuwa akianza kikosi cha kwanza, si katika nafasi ya kiungo, bali ni upande wa kulia nyuma, Hojbjerg akiwa mmoja wa makinda ndani ya kikosi hicho akamwambia kocha wake atakuwa mwenye furaha kucheza eneo lolote ambalo timu ingemhitaji.
Jiji la Berlin lilikuwa katika mwonekano tofauti, maelfu ya mashabiki waliuteka mji, makao makuu ya nchi yakawa kama bahari yenye rangi ya njano ambayo unaweza kuitofautisha kidogo kwa kialama chekundu kilichochomoza. Wachambuzi walionekana kuibeba Dortmund na vyombo vya habari ni hivyo hivyo waliiona ni timu iliyokuwa katika kiwango cha juu kiuchezaji.
Tayari Pep alikuwa na orodha ya kikosi chake pamoja na mpango mzima wa mechi husika, timu aliyoipanga ilionyesha azimio lake la anachotaka kukifanya msimu ujao. Alichagua wachezaji ambao wamekuwa wakijituma kwa sana katika falsafa yake ya kiuchezaji (majeruhi aliwaweka kando).
Mbinu ya siku ya mechi hiyo ilikuwa ni ile ya kuwapeleka hatua moja zaidi katika mabadiliko ya kiufundi ambayo Pep aliyasimamia ambayo alidhamiria kuona yanakuwa sehemu muhimu katika zama zake.
Ni saa mbili asubuhi, Jiji la Berlin lilikuwa na kimvua kidogo, kuna mambo mengi yanayoonekana kujitokeza zaidi ya mechi ya fainali ya Kombe la Ujerumani kati ya Bayern na Dortmund.
Baada ya kushindwa kutamba mbele ya Real Madrid kwenye ligi ya mabingwa, Pep amefanya badiliko moja muhimu ambalo linahusisha mambo mengi kwa upana na si suala la mbinu tu za kiuchezaji.
Ni mbinu za kimkakati ambazo amekuwa akizifanyia kazi kipindi kirefu, akifanyia tathmini nguvu na uwezo wa timu yake, Pep alihitimisha kwa kujiaminisha timu iko katika ubora kwa namna ambavyo wanaitumia vizuri mipira kwa kuanzia wachezaji watatu wa nyuma.
Katika hilo wanakuwa tayari wamejihakikishia walau mmoja wa mabeki ana nguvu na stamina ya kutoka kwenye mstari na kurudi nyuma au kupanda wakati wowote itakapolazimika, pia awe makini na maeneo aliyo karibu nayo.
Wakati huo huo, watakuwa wakimtumia kiungo aliye mbele ya mabeki wawili wa kati ambaye jukumu lake litakuwa ni kudhibiti mashambulizi ya kushtukiza ya timu pinzani na ambaye pia atakuwa tayari kurudi nyuma kuwasaidia mabeki wa kati pale atakapohitajika.
Pia atakuwa na mshambuliaji wa kati mwenye uwezo wa kuwafanya mabeki wanne wa timu pinzani wakae nyuma zaidi pamoja na mshambuliaji wa pili au kiungo mshambuliaji mwenye kuweza kucheza katika maeneo, pia atakuwa na ushirikiano mzuri na kiunganishi wa mshambuliaji wa kati.
Itaendelea Jumanne ijayo…