Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Simba ajuta kuitosa Yanga

Muktasari:

  • ·         Aliyekuwa kiraka wa Simba, Jamal Mwambeleko ameweka wazi kuwa alifanya makosa kujiunga na timu hiyo na kuipiga chini Yanga ambao walionyesha nia ya kuwa naye mapema.

BEKI wa zamani wa Simba, Jamali Mwambeleko ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo amekiri kuwa alizingua mwenyewe.

Mwambeleko alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mbao mwanzo wa msimu huu aliomba barua ya kuvunjwa kwa mkataba wake kwa kuwa alikuwa hapati nafasi ya kucheza.

Mwambeleko anasema kabla ya kusaini Simba viongozi wa Yanga walimfuata na kutaka asaini mkataba katika klabu yao.

“Nilishindwa kukubaliana nao kwa kwani walikuja mali kauli, lakini Simba walikuja na pesa mkononi ndio maana nikakubali kwenda kusaini,” alisema.

“Baadae nilikuja kuona kwamba nimezingua na huenda sikufanya uamuzi sahihi kwani kocha wa Yanga, George Lwandamina ndio alikuwa akinitaka zaidi kwa wakati huo.

“Huenda kutokufanya uamuzi sahihi zaidi lakini, Lwandamina hata alipoondoka nchini nilikuwa nikiwasiliana naye na kuniambia akipata timu Zambia yenye mahitaji ya mchezaji kama mimi ataniita, “ alisema Mwambeleko.

“Hata hapa KCB mkataba wangu upo wazi kama naweza kupata timu nyingine kabla ya mkataba kumalizika wanaweza kuniuza na hicho kilichangia nisisaini mkataba Gor Mahia kwani nao walikuwa wananihitaji kabla ya kuja hapa KCB, “ aliongezea.

Mwambeleko baada ya kupata barua hiyo kama mchezaji huru alitimkia Singida United ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 15 milioni.

Mwambeleko alikaa hapo Singida ndani ya mwezi mmoja tu akicheza mechi mbili dhidi ya Biashara United na African Lyon na aliondoka katika klabu hiyo kwa madai walishindwa kumtimizia mahitaji yaliyokuwa katika mkataba wake.