Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker afanya kilichomshinda Fadlu

Muktasari:

  • Ushindi huo wa Simba umemaliza unyonge wa misimu zaidi ya mitatu ya kutopata ushindi katika Ligi Kuu na mashindano mbalimbali.

KOCHA Steve Barker amefuta uteja wa Simba kwa Yanga baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa Simba umemaliza unyonge wa misimu zaidi ya mitatu ya kutopata ushindi katika Ligi Kuu na mashindano mbalimbali.

Barker amefanya kile kilichomshinda Msauzi mwenzake Faldu Davis wa kushindwa kuifunga Yanga katika michezo sita mfululizo aliokutana na watani zao hao.

Faldu msimu uliopita aliweka rekodi ya kuiongoza Simba kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza baada miaka 30, lakini kushindwa kuwapa raha Wanamsimbazi ni moja ya sababu iliyopelekea kutimuliwa mwanzoni mwa msimu uliopita.

Katika kuhakikisha wanamaliza uteja huo uongozi wa Simba ulimleta Barker mwishoni mwaka 2025, tangu ametua nchini ameiongoza Simba katika mechi nne akipata sare mbili na kufungwa mmoja na kushinda mmoja.

Katika mchezo wa jana Barker alionekana na mpango bora kuanzia mwanzo wa mchezo huku kucheza kwa kasi kuliwapa faida, licha ya kuruhusu bao la mapema kupitia Peter Shalilule.

Kipindi cha pili Simba ilirudi kwa kasi yake huku ikifaidika na kuumia kwa kiungo wa Yanga, Duke Abuya aliyeumia na nafasi yake kuchuliwa na Fred Ngoma.

Kiungo Neo Maema alifunga bao la kusawazisha la Simba akiunganisha krosi ya Libasse Gueye katika dakika 68.

Dakika mbili baadaye mshambuliaji Elie Mpanzu kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Yanga na pili kwa Simba katika mchezo huo akiwazidi kasi, beki Ibrahim Bacca kabla ya kumlamba chenga kipa Diarra na kufunga bao hilo la ushindi.

Mbali ya kuifunga Yanga, Barker pia kabla ya mapumziko ya Fifa aliifunga Azam kwa mabao 2-0 ikiwa ni ishara njema kwake kwa miamba hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.

Ushindi huo unaifanya Simba kukalia usukani wa ligi ikiwa na pointi 21 baada ya kushinda mechi zake saba huku Yanga wakibaki nafasi ya pili kwa pointi 18.

Kwa Wanasimba sasa ndoto yao ni kuiona timu yao ikiendelea na kasi hiyo hadi kutwaa ubingwa wa ligi walioupoteza kwa zaidi ya misimu mitano mbele ya watani zao Yanga.