Bandari SC yatambulisha 15, Lomalisa atajwa kutua
Muktasari:
- Baada ya kupanda kutoka First League, timu hiyo ina mipango ya kufanya usajili wa nguvu ili kuleta ushindani katika ligi hiyo.
NYOTA wa zamani wa Yanga aliyesifika kwa krosi na kubatizwa jina la ‘Waziri wa Maji’, Joyce Lomalisa anatajwa kutua katika timu ya Bandari SC itakayoshiriki Ligi ya Championship Bara 2026/27.
Baada ya kupanda kutoka First League, timu hiyo ina mipango ya kufanya usajili wa nguvu ili kuleta ushindani katika ligi hiyo.
Hadi sasa kikosi hicho kimetambulisha nyota 15 wapya wakiwamo Ambokise Mwaipopo, Ibrahim Koba, Haji Ugando, Jabir Masumbuko, Jofrey Kigi, Joe Makoye na Ayoub Semtawa.
Wengine ni Isah Ngoah, Selemani Omary, Willium Elias, Abdul Hilary, Razack Shekimweri, Ally Ramadhani, Denis Tamba na Miza Abdallah.
Ligi hiyo inatarajiwa kuanza wakati wowote kati ya sasa na Septemba, mwaka huu.