Azam yapewa mfupa mgumu Afrika, Singida BS angalau
Muktasari:
- FAR Rabat msimu uliopita ilitinga hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupoteza dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Azam FC imepangwa katika kundi C la Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Katika droo iliyomalizika dakika chache zilizopita leo Jumatano, Oktoba 28, 2026 jijini Cairo, Misri, Azam imepangwa na timu za FAR Rabat ya Morocco, Al Ahli Tripoli ya Libya na Durban City ya Afrika Kusini.
FAR Rabat msimu uliopita ilitinga hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupoteza dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Pia imewahi kutwaa taji moja la Ligi ya Mabingwa Afrika na moja la Shirikisho Afrika.
Al Ahli Tripoli imewahi kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2021/2022.
Durban City hii ndio mara yake ya kwanza kucheza hatua ya makundi.
Singida Black Stars yenyewe imeangukia katika kundi C lenye timu za CR Belouizdad ya Algeria, AS Maniema Union ya DR Congo na Red Arrows ya Afrika Kusini.
Ni CR Belouzdad pekee kwenye kundi hilo ambayo angalau imewahi kufika hatua za juu za mashindano ya klabu Afrika.
Mwaka 1996, timu hiyo ilifika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Washindi Afrika.