70 Betika mtoko wa kibingwa uhakika Kariakoo dabi
Mabingwa 70 wamejihakikishia kushuhudia dabi ya Simba na Yanga ya Aprili 16 jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa mabingwa hao wa Betika mtoko wa kibingwa ni wa kutoka Dar es Salaam ambao tayari 20 wamefanyiwa usaili huku 50 kutoka mikoa mingine wakikabidhiwa tiketi za ndege tayari kwenda Dar es Salaam kuishuhudia dabi hiyo.
Ofisa habari wa Betika, Juvelinaus Rugambwa alisema mabingwa wa Dar es Salaam wanaendelea na usajili na siku chache kabla ya mechi hiyo ya dabi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara wataungana na wale wa mikoani tayari kuishuhudia kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, wakigharamiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Betika Tanzania.
"Tumebakiza washindi 30 kuhitimisha droo hii, hadi sasa tuna washindi 70 kati ya 100 wa Mtoko wa kibingwa msimu huu kutoka kote nchini, bado nafasi zipo kwa watu 30, wanachotakiwa ni kuweka mikeka mitano ya kuanzia Sh 500," amesema na kuongeza.
"Aprili 3 droo nyingine ya washindi itafanyika, tunatarajia kuwa na droo ya mwisho Aprili 10.
"Ni rahisi kushinda kwa kuweka beti za mikeka mitano kwa siku ya kuanzia Sh 500 bila kujali mkeka umechanika au la moja kwa moja unaingia kwenye droo ya mtoko wa kibingwa,".
Amesema siku moja kabla ya dabi hiyo, washindi wote 100 watashiriki hafla ya bata la mtoko litakalofanyika Kidimbwi sanjari na kuwasikiliza wachambuzi mahiri watakaochambua mambo kadha wa kadha kuelekea kwenye dabi hiyo ya lala salama ya Ligi Kuu.
"Kwenye bata la mtoko kutakuwa pia na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii maarufu nchini wakiongozwa na Christian Bella," amesema.