Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utajiri wa Mo Dewji unatisha

Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ametajwa kushika nafasi ya 13 katika orodha ya watu 18 tajiri barani Afrika inayoongozwa na Taikuni wa Nigeria, Aliko Dangote.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida maarufu la Forbes, Dewji (45) anashika nafasi hiyo akiwa na utajiri unakadiriwa kufikia Dola 1.6 bilioni (Sh 3.7 trilioni) zilizotokana na uwekezaji wake katika biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali.

Uwekezaji katika viwanda vya nguo, unga wa ngano na sembe, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari na vinywaji unatajwa kama chanzo cha utajiri huo wa Dewji ambaye kwa hapa Tanzania yeye pekee ndiye ameingia katika orodha hiyo ya mataikuni 18 barani Afrika.

Kwa kuingia katika orodha hiyo, Dewji anafuata nyayo za Mmiliki wa Mamelodi Sundowns, Patrice Motsepe amabye yeye ana utajiri unakadiriwa kufikia Dola 3 bilioni (zaidi ya Sh 9 trilioni)

Pia Dewji ndiye mtu pekee kutoka Afrika Mashariki aliyeweza kuingia katika orodha hiyo kwa mujibu wa Forbes huku nchi za Afrika Kusini, Nigeria na Misri zikitawala.

Aliko Dangote aliyewekeza katika biashara za sukari na simenti anashika nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa Dola 12.1 bilioni na anafuatiwa na Nassef Sawiris kutoka Misri mwenye utajiri wa Dola 8.5 bilioni huku nafasi ya tatu ikishikilia na Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 8 bilioni.

Wanaofuatia katika orodha hiyo na utajiri wao kwenye mabao ni Nicky Oppenheimer (Dola 7.2 bilioni), Mike Adenuga (Dola 6.3 milioni), Abdulsamad Rabiu (Dola 5.5 bilioni), Issad Rebrab (Dola 4.8 bilioni), Naguib Sawiris (Dola 3.2 bilioni), Patrice Motsepe na Koos Bekker (Dola 2.8 bilioni).

Wengine ni Mohamed Mansour (Dola 2.5 bilioni), Aziz Akhannouch (Dola 2 bilioni), Youssef Mansour (Dola 1.5 bilioni), Othman Benjelloun (Dola 1.3 bilioni), Othman Benjelloun (Dola 1.2 bilioni), Strive Masiyiwa (Dola 1.2 bilioni) na Yasseen Mansour (Dola 1.1 bilioni).