Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi: Ikambi Mungu anakuona!

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi hana raha kutokana na kupewa kadi nyekundu inayomfanya akose mechi tatu ikiwamo dhidi ya Simba na kasema hajui kilichomfanya mwamuzi Raphael Ikambi kumpa, akimwambia ajue Mungu anamuona kwa kumuadhibu bila hatia.

Mwamuzi huyo alimlima Nabi dakika za lala salama za mechi ya robo fainali ya Kombe la ASFC dhidi ya Geita Gold kwa ushauri wa mwamuzi wa akiba, Heri Sasii na kocha huyo alisema tangu aanze kufundisha soka Ikambi amemtibulia rekodi yake.

Nabi alisema hakuna mwamuzi aliyewahi kumtolea lugha chafu tangu aanze kufundisha soka na hata hapa nchini licha ya kukutana na uamuzi uliomshangaza.

Alisema alimfuata Sasii kumuuliza juu ya mchezo kumalizika mapema hali ya kuwa kuliongezwa dakika tano za nyongeza, huku ndani yake muda mrefu ukitumika kumtibu beki wa Geita aliyeumia dakika za mwisho.

“Sijajua kipi nilimkosea, nimekuwa nikijiuliza sipati jibu. Sina rekodi ya kuwatusi waamuzi tangu nimefika hapa, kumekuwa kukitokea uamuzi wenye utata lakini sijawahi kufanya vitu vya hovyo,” alisema Nabi.

“Nilimfuata mwamuzi wa akiba (Sasii) nikamuuliza imekuwaje dakika zilionyeshwa tano na tumetumia kama tatu pekee? Sijui hapa alikasirishwa na kipi wakati kila mtu aliona jinsi mchezo uliposimama yule mchezaji wao (Geita Gold) alipokuwa anatibiwa.”

Akizungumzia mabadiliko ya ratiba, Nabi alisema hatua hiyo ni nzuri kwa kikosi chake ambapo itakwenda kuwapa nguvu ya kimaandalizi kuelekea mchezo wa Simba utakaopigwa Aprili 30.