Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Morihno' aibukia Mashujaa Queens kuanza na Simba Queens

Muktasari:

  • Mashujaa Queens kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu ikiwa na pointi sita.

Siku moja kabla ya Mashujaa Queens kuivaa Simba Queens katika Ligi Kuu ya Wanawake, timu hiyo imemnasa rasmi Kocha Edna Lema.

Leo Jumanne, Novemba 11, 2026, Mashujaa Queens imemtangaza Edna Lema ‘Mourinho’ kuwa Kocha wake Mkuu mpya.

Kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na kibarua chake cha kwanza ni mchezo huo dhidi ya Simba Queens kesho Jumatano, Novemba 11, 2026 katika Uwanja wa Mej. Jen Mzee, Dar es Salaam.

“Karibu kwenye himaya ya Kishujaa Edna Lema ‘Mourinho’,” imesema taarifa ya Mashujaa FC.

Kocha huyo mwenye leseni A ya Ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amejiunga na Mashujaa Queens baada ya siku 42 kupita tangu alipoachana na Yanga Princess.

Edna alijiondoa Yanga Princess baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 3-0 katika mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Septemba 30, 2026.

Akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi baada ya kumwaga wino Mashujaa Queens, Lema amesema kuwa kiu yake ni kuipandisha timu hiyo kimafanikio.

“Mara kadhaa Mashujaa Queens imemaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi sasa tunahitajika kusogea nafasi za juu zaidi na hasa kutwaa ubingwa.

“Ni jambo linalowezekana kwa vile timu ina wachezaji wazuri,” amesema kocha huyo.

Mashujaa Queens kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu ikiwa na pointi sita.