Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Tabora United ahesabiwa saa

Muktasari:

  • Habari za ndani ambazo Mwanaspoti limezinasa kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya timu hiyo ni kwamba uongozi ulikutana na kocha na kumjulisha uamuzi wa kuachana naye na sasa umeanza mchakato wa kusaka mpya.

NI suala la muda tu lililobakia kwa Tabora United ya mjiani Tabora kutangaza uamuzi mgumu wa kuachana na kocha Goran Kopunovic kutoka Serbia kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu.

Habari za ndani ambazo Mwanaspoti limezinasa kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya timu hiyo ni kwamba uongozi ulikutana na kocha na kumjulisha uamuzi wa kuachana naye na sasa umeanza mchakato wa kusaka mpya.

“Mambo mengi yamekuwa hayaendi sawa kwenye timu lakini kubwa zaidi ni muendelezo wa kufanya vibaya ambao tumekuwa nao uliopelekea tuwe katika nafasi ya hatari kwenye msimamo wa ligi.

“Kuna baadhi ya taratibu ambazo uongozi unazikamilisha kabla ya kutangaza rasmi uamuzi wa kuachana na kocha ambazo zikiwekwa sawa mambo yatakuwa hadharani,” kilifichua chanzo.

Alipotafutwa kuzungumzia taarifa hizo, Mtendaji Mkuu, Thabit Kandoro alisema Kopunovic ni kocha wa Tabora United.

Licha ya ufafanuzi huo wa Kandoro, Mwanaspoti linafahamu kuwa mchakato wa kumsaka kocha mpya umeshaanza na ukikamilika ndipo timu hiyo itatangaza kuachana na Kopunovic.

Katika mechi 21 ilizocheza kwenye Ligi Kuu, Tabora United imepata ushindi mara nne tu, ikitoka sare tisa na kupoteza michezo saba.

Safu ya ushambuliaji inaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kumuangusha Kopunovic kwani imefunga mabao 15 ambayo imeyapata katika mechi 11 huku ikifumania nyavu katika mechi tisa tu.

Wakati ikiwa na safu dhaifu ya ushambuliaji, timu hiyo bado inahaha katika upande wa ulinzi kwani hadi sasa imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 25 katika Ligi Kuu Bara.

Tabora United imebakiza mechi tisa dhidi ya JKT Tanzania, Kagera Sugar, Geita Gold, Mtibwa Sugar, Simba, Mashujaa, Ihefu, Yanga na Namungo.