Kiraka Mbao FC atua kuipa nguvu KMC
Muktasari:
- Sadala alikuwa akiitumikia Mbao akitokea Azam , lakini baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo ameamua kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia KMC inayonolewa na kocha Ettiene Ndayiragije aliyewahi kumfundisha akiwa Mbao.
- Sadala aliliambia Mwanaspoti sababu kubwa yakuamua kusaini kuitumikia timu hiyo ni baada ya kulidhishwa na mipango yao ambayo wamejiwekea katika msimu ujao wa Ligi Kuu.
TIMU ya Halmashauri ya Manispaa Kinondoni (KMC), imeendelea na usajili baada vya kufanikiwa kudaka saini ya kiraka wa Mbao, Sadala Lipangile.
Sadala alikuwa akiitumikia Mbao akitokea Azam , lakini baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo ameamua kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia KMC inayonolewa na kocha Ettiene Ndayiragije aliyewahi kumfundisha akiwa Mbao.
Sadala aliliambia Mwanaspoti sababu kubwa yakuamua kusaini kuitumikia timu hiyo ni baada ya kulidhishwa na mipango yao ambayo wamejiwekea katika msimu ujao wa Ligi Kuu.
“Kusaini kwangu hapa ni baada ya kuona kwamba ni timu inayotafuta kitu, sio kwamba ni kwa haraka lakini wamejiandaa kabisa unaona wanakitu wanakitafuta, lakini vile vile kuelewana kwangu na mwalimu ambapo nilifanya nae kazi vizuri,” alisema.
Akizungumzia kuhusu changamoto katika timu kama Kmc ambazo zinakuwa na presha nkubwa baada ya kupanda na kutaka kufanya mageuzi makubwa, alisema changamoto anachukulia kama moja ya motisha yay eye kufanya vizuri.
“Changamoto au presha sio kitu cha kukiogopa hata kidogo kwasababu hata Mbao nilikuwa katika wakati huo na ni timu ambayo ilikuwa na presha kubwa hasa tukifanya vibaya, lakini niliweza kujitahidi kuvumilia kikubwa najipanga niweze kufanya vizuri katika msimu ujao nikiwa hapa,” alisema.