Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ISHU YA SARPONG IPO HIVI...

Kocha wa Yanga, Cedrick Kaze alielezea uwepo wa washambuliaji wake kikosini, Michael Sarpong na Waziri Junior licha ya awali kuonekana wangeondoka kwenye timu hiyo dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15 kutokana na kutoonyesha kiwango cha juu.

Kaze alisema aliamua kutoruhusu Sarpong aondoke na Junior atolewe kwa mkopo kwenda timu nyingine kwa sababu anahitaji ushindani, pia ili apate fursa ya kutafuta suluhisho la udhaifu wao.

“Yanga ni timu kubwa na inayohitaji wachezaji washindani na sidhani ni sahihi kwa mchezaji kukimbia ushindani wa namba, hivyo nikataka wabaki washindane.Ukisema kila unapokosa nafasi basi uondoke kwenda kwingine sidhani kama ni sahihi na hata kwa wao wanapaswa kushindana,” alisema Kaze na kuongeza;

“Nimesikia baadhi ya watu wakilalamika juu ya kiwango cha baadhi ya wachezaji lakini niko nao mazoezini na najua mchango na ufanisi wa kila mchezaji. Mfano Songne Yacouba hakuwa anafanya vizuri alipokuwa akipangwa kama mshambuliaji wa kati.

“Baada ya kumpanga winga wa kushoto mechi dhidi ya Azam hadi sasa, amekuwa akifanya vizuri na amefunga mabao manne katika mechi kama sita au saba hivi zilizopita jambo linaloisaidia timu.Sasa kuna wakati pia upande wa makocha tunapaswa kujifanyia tathmini wenyewe juu ya ufanisi wa wachezaji wetu. Maana inawezekana tatizo linaanzia kwetu,” alisema Kaze.

Kocha huyo alisema anaamini programu wanazoendelea kufanya pamoja na usajili walioufanya katika dirisha dogo vitasaidia kuleta chachu ya ushindani na kuimarisha kikosi chao.

“Mchezaji kama Fiston tumemsajili aje kuungana na wenzake na kwa kuangalia uzoefu wake naamini ataongeza kitu kwenye timu, pia wigo kwa benchi la ufundi pasipo kuathiri timu,” alisema Kaze.