Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam wamshusha straika wa Yanga, Simba

AZAM wanajisuka taratibu tena kimyakimya na sasa jamaa wamemshusha kimyakimya mshambuliaji mmoja ambaye aliwashinda Simba na Yanga.

Azam jana mchana Desemba 22, 2020 walimshusha nchini mshambuliaji, Mpiana Mozizi kutoka DR Congo akitua kimyakimya kuja kuungana na timu hiyo ambayo imeyumba katika mechi kadhaa za Ligi Kuu kiasi cha mashabiki kujiuliza kulikoni?.

Mapema kocha mpya wa timu hiyo George Lwandamina aliliambia Mwanaspoti kuwa anahitaji kuongeza mshambuliaji mmoja,kiungo na kipa katika kukirudishia makali kikosi hicho baada ya kumkosa Prince Dube ambaye ni majeruhi.

Wakati wa dirisha kubwa la usajili Simba na Yanga zilikumbana kwa mchezaji huyo lakini zikaishia kusonya baada ya kulishindwa dau lake. Wakati ule alitaka dola 60,000 sawa na Sh 138mil.

Taarifa ambazo Mwanaspoti ina uhakika nazo ni kwamba Mozizi ambaye alikuwa mmoja wa wafungaji bora msimu uliopita katika Ligi Kuu ya nchini Congo ametua jana na sasa yumo ndani ya mikono ya mabosi wa Azam ambao wamekuwa wasiri kutaja dau lake.

Jana mchana Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkarim Popat alionyesha dalili za ujio wa mshambuliaji huyo akiweka picha ya bendera ya DR Congo kwenye mitandao ya kijamii.

Bosi mmoja wa FC Lupopo ya Congo ameliambia Mwanaspoti kuwa mshambuliaji huyo ameshaondoka nchini kwao. ; “Unajua Mpiana alikuwa hapa kwa mkopo akitokea klabu yake ya Rangers sasa naona rais wa klabu yake ameshakubaliana na Azam na ameondoka hapa yuko Tanzania.”

“Aliondoka hapa Congo kwa kificho sana unajua mashabiki wa hapa wana vurugu sana wakisikia mchezaji mkubwa anaondoka nasikia aliondoka kwa siri sana ili mashabiki wasijue mtafute hapo Tanzania utamuona,”alisema ingawa Azam jana walikuwa wakifanya siri kubwa.