Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumefuzu kiandamizi sana 16 Bora AFCON 2025

SHABI 01

Muktasari:

  • Ndio, tumefuzu lakini kwa namna ya kushangaza kidogo, kwani tumepenya kupitia njia ya timu nne zenye matokeo bora ambazo zilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye misimamo ya makundi yao.

BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye ndoto yetu Tanzania kuona timu ya taifa, Taifa Stars inafuzu hatua ya mtoano ya Fainali za AFCON imetimia juzi Jumanne.

Ndio, tumefuzu lakini kwa namna ya kushangaza kidogo, kwani tumepenya kupitia njia ya timu nne zenye matokeo bora ambazo zilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye misimamo ya makundi yao.

Katika hao wanne, nasi tumo japo tumemaliza tukiwa na pointi mbili lakini zimetosha kutupeleka hatua ya 16 bora ambayo ndio tumeingia kwa mara ya kwanza.

Haijalishi tumeingia hatua ya robo fainali au hatujafanya hivyo, kijiwe kinaamini hayo ni mafanikio makubwa kwetu kwa vile tumefikia lengo letu ambalo lilikuwa ni kufika 16 bora ambayo sasa tushaingia.

Hapo katika hatua ya 16, tunakutana na wenyeji Morocco, ambao ndio timu namba 1 katika ubora wa viwango Afrika na pia timu pekee ya bara hili iliyowahi kufika nusu fainali ya Kom be la Dunia, ikafanya hivyo katika fainali zilizopita kule Qatar 2022.

Kitendo cha kufuzu huku tukiwa tumepata pointi mbili tu katika hatua ya makundi kituamshe na kiendelee kutukumbusha kwamba maisha katika AFCON yamebadilika na sasa kuishia hatua ya makundi sio jambo la kupendeza au la kujivunia.

Kufuzu kunatakiwa kutupa chachu ya kuhakikisha katika fainali zijazo ambazo zitafanyika hapa nchini, Kenya na Uganda tunafanya vizuri zaidi.

Tupambane tukusanye pointi za kutosha katika hatua ya makundi 2027 ili tusiingie katika mtego wa kutegemea besti luza kama ilivyotokea mwaka huu.

Huku kufuzu kiandamizi tusidhani kama tutakuwa tunafanya hivyo kila wakati ambao Fainali za AFCON zitakuwa zinafanyika.

Yote kwa yote, Taifa Stars tumeutua mzigo ambao tuliubeba kichwani wa kushindwa kufuzu hatua ya mtoano katika fainali za Afrika na kuanzia sasa lengo litakuwa robo fainali au hatua za juu zaidi.