Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapya hali ngumu Junguni United

JUNGUNI Pict

Muktasari:

  • Mbali na mchezaji huyo, viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu na Shirikisho la Soka Zanzibar wameamua kuingilia kati.

BAADA ya Aprili 27, 2026 gazeti hili kuripoti hali ngumu inayopitia Junguni United inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), mapya yameibuka huku mmoja wa wachezaji akieleza mazito ikiwemo sababu ya kuondoka klabu kambini kabla ya msimu kumalizika.

Mbali na mchezaji huyo, viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu na Shirikisho la Soka Zanzibar wameamua kuingilia kati.

Taarifa hiyo ilieleza baadhi ya wachezaji wa Junguni waliosajiliwa dirisha dogo msimu huu wameondoka kabla ya msimu kumalizika kwa madai ya hali ngumu iliyosababishwa na hali ya kiuchumi.

Na taarifa hiyo ilieleza kuna wasiwasi wa Junguni kutosafiri kwenda Unguja kutoka Pemba kwa ajili ya kucheza mechi mbili za raundi ya 25 na 26 kwani fedha hakuna, huku msemaji wa timu hiyo, Suleiman Mwinyi Hamad akisema: "Timu imeshindwa kujiendesha kutokana na ukosefu wa fedha jambo ambalo limebabaisha kuomba msaada kwa wengine bila mafanikio.

"Fedha ndiyo chanzo kikuu cha migogoro ndani ya timu kwani kila mmoja ana mtazamo wake hususan fedha zinazoingizwa na mdhamini wa ligi."

VIONGOZI WAFUNGUKA
Mbunge wa Jimbo la Gando, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salim Mussa Omar, ambako timu hiyo ipo ameliambia Mwanaspoti kuwa, ameshangazwa na taarifa za Junguni kufikia hatua ya wachezaji kukimbia hali ngumu ya maisha wakati kuna utaratibu ulioweka wa viongozi wa klabu hiyo walipaswa kuufuata kukabili suala la kiuchumi hiyo.

"Sijasitisha kuwasaidia, mimi jimboni nimeweka mtu ambaye kama wakiwa na shida yoyote wakienda wanapatiwa msaada. Mara ya kwanza walipata, mara ya pili wakaenda wakapeleka bajeti ya i-wakapata, sasa sijui nini kimetokea.

"Nina wasiwasi kuna muungano ya viongozi. Mwanzo nilipokuwa nawasaidia fedha wao moja kwa moja ilifikia wakati ukimtumia kiongozi A, basi kiongozi B anakwambia mara nyingine usitume huko.

"Sulukisho nikaona nimuweke mtu maalum ambaye jina lake anaitwa Abdrahman Ali Nuhu weke huyo mtu hawajawahi kwenda wakakosa msaada," alisema mbunge huyo.

Ili katua changamoto hiyo, mbunge huyo alitoa ushauri akisema: "Wakae chini wachague uongozi bora ambao utakubali kufanya kazi kwa kushirikiana."

Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), Hamis Juma alisema suala hilo la Junguni halijafikiana kwake zaidi ya kuliona kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo, alitolea ufafanuzi wa matumizi ya fedha ambazo hupewa klabu na mdhamini mkuu kwa ajili ya ushiriki wa Ligi Kuu Zanzibar.

"Watakapokuja katika ofisi yetu bila shaka watahojiwa kwa nini wamepewa pesa na wameshindwa kuzitumia kwa utaratibu wakamaliza kile ambacho kilikusudiwa, majibu yao ndiyo yataratibu nini cha kufanya," alisema.

Aliongeza kuwa shirikisho limekuwa likifanya juhudi ili kuhakikisha klabu zinakuwa vizuri kiuchumi na wamekuwa wakizungumza kwa karibu na wadhamini wengine.

"Kila klabu inapewa Sh35 milioni, sisi wajibu wetu tayari tumefanya, sasa mengine yaliyobaki ni jukumu lao," alisema.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali aliliambia Mwanaspoti kuwa: "Fedha zinafteremshwa kwa sababu klabu hujapewa nyingine unatakiwa utoe maelezo ya matumizi yale. Kwa hiyo wanaleta mrejesho kwa mujibu wa tamtibu za fedha, hapo ndipo wanapatiwa nyingine."

Kuhusu hatua wanazochukua ikitokea klabu ikatumia fedha za udhamini tofauti na maelekezo, mtendaji huyo alisema: "Kama itatokea hivyo, utaratibu zitachukuliwa kulingana na masharti na makubaliano ya mdhamini.

"Sisi tunawapatia mafunzo ya usimamizi wa wahakikishe kila klabu iwe na mdhamini wake angalau mmoja wa saba sababu mdhamini wa sasa amekana kushiriki katika uendeshaji wa vitu vingine kama usafiri."

Mtunza Fedha wa Junguni United, Hamis Kombo Mussa, aliliambia gazeti hili kuwa kuna baadhi ya viongozi ndani ya klabu hiyo sio waaminifu na ndiyo wamesababisha hali kuwa ilivyo.

"Kuna kiongozi (anataja jina) hali mkweli wala mwaminifu na ndio chanzo kikuu cha uongozi wa timu hii kuvurugika na kwa sasa viongozi wengi wameachia timu kwa sababu yake," alisema.

Alisema awali timu hiyo ilikuwa inasaidiwa na mbunge wa Gando, lakini baada kuona viongozi waliopo sio sahihi akaamua kusitisha.

Awali, Mwanaspoti lilifanya juhudi za kumtafuta Katibu wa Junguni, Suleiman Mwidani Asaa, ambapo alisema yupo Wete, lakini akamwambia mwandishi kama akiridhika na maelezo atalayopewa klabuni, hakuna shida, Ndipo mwandishi akaefika klabuni na kuzungumza na baadhi ya viongozi waliokuwepo na kueleza hali halisi inayoendelea.

Baadaye alipotafutwa Mwenyekiti wa Junguni United, Shibu Sharif Omar kwa njia ya simu, kwanza alisema klabu hiyo ina viongozi wawili waliochaguliwa ambao ni yeye na katibu, kisha kuna wajumbe walioteuliwa.

Alisema masuala ya kuuzungumzia klabu hiyo yapo chini ya viongozi hao wawili, lakini alipoulizwa endapo wao hawapo ofisini na wajumbe waliowateua wapo, alidai taarifa wanazotoa ni sehemu ya kuwakakilisha wao.

Alipoulizwa kuhusu kinachoendelea klabuni hapo hadi kuwepo madai ya baadhi ya wachezaji kuondoka kutokana na hali ngumu ya maisha, alisem: "Hayo ni mahojiano ambayo mimi si kazi yangu kulupia, Kama wapo au hawapo natakiwa nijue mimi na hata kama wewe unajua basi utakuwa unajua kwa nafasi yako."

MSIKIE MCHEZAJI
Akizungumza na Mwanaspoti, Nature Mwakilembe ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa Junguni United walioondoka kwa madai ya hali ngumu, alisema alishindwa kuvumilia ilamlazimu kuomba msaada msikitini ili apate nauli ya kurudi Mbeya.

"Nilivyoona viongozi wa timu hawatoi ushirikiano kwetu ndipo nilipoamua niende msikitini kuomba msaada," alisema.

Nature alisema, baada ya kufika msikitini kuomba msaada alipatiwa kiasi cha Sh80,000, akapiga kwa nauli iliyomtoa Pemba hadi Dar na alipofika ilimlazimu kuwagawia simu ndugu zake wamtumie nauli ndipo akasafiri hadi Mbeya alipo kwa sasa.

Alisema aliamua kuomba msaada wa kurudi kwao akiamini atakapokuwa nyumbani hakuna jambo ambalo litaharibika kwani angekuwa na uwezo wa kucheza hata mechi za mtaani kujipatia fedha za kuendesha familia yake.

Kuhusu maisha ndani ya Junguni United, Nature alisema ilifikia wakati wachezaji wakawa wanakula mlo mmoja.

Alisema licha ya mazingira magumu waliyopitia, lakini waliendelea kucheza kwa na timu nyingine lakini hali ilivyozidi, uvumilivu ulimshinda.

"Nilishindwa kustaifiri milivyona hata hela ya chakula ni changamoto niliwapingia viongozi tukae chini tuone namna ya kuiendesha timu, lakini hawakutaka kutoa ushirikiano," alisema.

Nature aliyejiunga na Junguni United kipindi cha usajili wa dirisha dogo msimu huu, alisema baada ya kucheza mechi mbili dhidi ya KVZ na New King, alianza kuelewa maisha halisi ya klabu hiyo tangu wakiwa Unguja kabla ya kurejea Pemba.

Alisema kutokana na changamoto hiyo, baadhi ya wachezaji alioingia nao dirisha dogo la usajili walirejea Tanzania Bara wakitokea Unguja.

Nature alisem hali ambayo ilimsikitisha zaidi ni wakati alipopata majeraha ya kupasuka kichwani kwenye mechi ya Ligi Kuu Zanzibar dhidi ya JKU, ni walipopoteza kwa mabao 8-0 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, Aprili 18, 2026.

Alisema baada ya kupata jeraha hilo zilipita siku mbili bila ya kupata huduma yoyote na alipoomba Sh5,000 za matibabu, hakupatiwa.

Sasa Ligi Kuu Zanzibar inaendelea, ambapo imesimama kwa muda kupisha mechi za Kombe la FA.