Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi ndiyo sababu za Ibenge kukata mastaa Azam

Muktasari:

  • Chanzo chetu kinasema Ibenge anataka kubaki na wachezaji ambao anaamini watampa matokeo.


Baada ya kukaa na kikosi kwa mwezi mzima, kocha mkuu wa Azam FC amefyeka wachezaji kadhaa wa timu hiyo. Taarifa za kuaminika kutoka kwa watu wa karibu wa benchi la ufundi la kocha huyo zinasema Ibenge anaona wachezaji wengi katika kikosi hicho hawawezi kumsaidia kufikia malengo aliyopewa.


Japo majina rasmi hayajatajwa lakini inasemekana nahodha Sospeter Bajana na Wakolombia wawili, Jhonier Blanco, Ever Meza, Frank Tiesse na Mamadou Samake ni miongoni mwao.

Pia kuna wachezaji wengine kadhaa ambao kocha Ibenge anatilia shaka uwezo.


Miongoni mwao ni wachezaji wapya kama Mukhsini Malima, Himid Mao na Pape Doudou Diallo. Pia wapo wachezaji wa zamani kama Yeison Fuentes na James Akaminko.


SOSPETER BAJANA

Bajana ambaye ni zao la akademi ya Azam FC akiingia mwaka 2011, haingii kwenye mfumo wa kocha huyo raia wa Ufaransa mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Na tatizo la Bajana sio uwezo wake wa uwanjani bali kimo chake.

Bajana ana urefu wa futi 5.4 na Ibenge ni muumini wa wachezaji warefu katika nafasi za kati na amekuwa akiwatumia katika timu zake zote. Alipokuwa AS Vita alikuwa na Fabrice Ngoma (futi 6.2), Eddy Emomo (futi 6.1) na Nelson Munganga (futi 6).

Ngoma na Munganga pia ndio waliomsaidia Ibenge kushinda Kombe la.CHAN mwaka 2016 akiwa na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Akiwa Berkane alikuwa Larbi Naji (futi 6.2), Bakr El Helali (futi 6.1), na Sofian El Moudane (futi 5.8).

 Alipokuwa Al Hilal pia alikuwa na watu kama Aprocius Peter (futi 6), Guessouma Fofana (futi 6.1), Walieldin Khidir maarufu kama Pogba (futi 6.3) na huyu alimtaka anamtaka sana aje naye Azam lakini ikashindikana, ndio akamchukua Sadio Kanoute mwenye futi 6.1.

Kwa namna yoyote ile Bajana sio aina ya viungo wanaoingia kwenye timu ya Ibenge hata awe na uwezo wa aina gani.


WAKOLOMBIA

Jhonier Blanco na Ever Meza ambao walibeba matarajio makubwa, sio sehemu ya kikosi cha kocha Ibenge msimu ujao. Kocha huyo hawataki wachezaji hawa kwa sababu hawajitumi wanacheza kwa kuridhika sana. Kwa malengo ambayo klabu imempa, Ibenge anadhani anahitaji wachezaji watakaokuwa tayari kuteseka uwanjani.

Wakolombia hawa hawaoneshi jitihada zozote mazoezini na kutoa ishara kwamba hata kwenye mechi hawatomsaidia.


MMADOU SAMAKE NA FRANK TIESSE

Maeneo wanayocheza yamejaa watu wenye uwezo zaidi yao. Samake ni kiungo wa kati na Tiesse ni winga huko kumejaa sana na Ibenge anaamini ni matumizi mabaya ya nafasi za wachezaji kigeni kuendelea kuwa na wachezaji ambao hawatopata nafasi katika kikosi.


WENGINEO

James Akaminko na Yeison Fuentes ni wachezaji anaowatazama hadi Desemba. Kwanza ni vimo vyao lakini pili ni uwezo wao. Tangu amefika hawajamuonesha kitu kikubwa cha kumuaminisha kwamba wanaweza kumsaidia kutimiza malengo yake. Ila kwa kutazama video za mechi za msimu uliopita, anaona wana uwezo hivyo anawapa muda hadi Desemba, kuthibitisha uwezo wao.


WAPYA

Pape Doudou Diallo, Himid Mao na Mukhsini ni wachezaji waliosajiliwa msimu huu lakini anaona hawatoshi. Tofauti na akina Himid na Malima ambao alikuta tayari klabu imewasajili, Pape Doudou Diallo ni mchezaji aliyemchagua yeye mwenyewe lakini katika mwezi mmoja aliokaa naye kambini anahisi sio mchezaji mpambanaji.

Katika wachezaji wote aliowakuta, Ibenge amemuelewa zaidi Yahya Zayd hata kufikiria kumpa kitambaa cha unahodha. Zaidi ya hapo anawasubiri wachezaji walioko timu ya taifa, hasa wale waliokuwa wakicheza wale waliokuwa benchi anataka awatathmini zaidi Chanzo chetu kinasema Ibenge anataka kubaki na wachezaji ambao anaamini watampa matokeo.