Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Heels ‘mchuchumio’ Usipovaa vizuri haya ndiyo madhara yake

Muktasari:

  • Lakini hebu viatu hivyo vikianza kulipa kisasi baada ya sherehe, ndipo mwenyewe anaweza kujiuliza:

UKIMWONA mwanamke akikatiza kwenye hafla akiwa na heels ndefu, hatua zake zikigonga sakafu kwa kujiamini, ni rahisi kuamini kuwa kisigino kirefu ni siri ya mwisho ya kumalizia urembo wa mavazi.

Lakini hebu viatu hivyo vikianza kulipa kisasi baada ya sherehe, ndipo mwenyewe anaweza kujiuliza:

“Hivi nilikuwa nimevaa kiatu au nilikuwa nimejifungia adhabu miguuni?”

Heels (kiatu cha mchuchumio) zinaweza kuongeza mvuto wa mwonekano, lakini urefu na muda wa kuzivaa vinaweza kuongeza mzigo kwenye miguu, vifundo, magoti na hata mgongo.

Wataalamu wa afya ya miguu wanaonya kuwa kisigino kirefu husogeza uzito wa mwili kuelekea mbele ya mguu, huku viatu vyenye ncha finyu vikibaniza vidole.

INCHI NGAPI NI SALAMA?

Kama unataka kuvaa heels mara kwa mara, urefu wa kisigino ni jambo la kwanza kuangalia. Chaguo linalofaa zaidi kwa matumizi ya kawaida ni kisigino kifupi, takribani robo tatu ya inchi au karibu sentimita mbili.

Kwa anayehitaji kisigino kirefu zaidi, wataalamu wanashauri kuchagua kisigino kilicho chini ya inchi mbili, yaani karibu sentimita tano, na kiwe kipana na imara.

Kisigino cha zaidi ya inchi mbili kinaweza kuongeza shinikizo kwenye sehemu ya mbele ya mguu. Wataalamu pia wanaonya kuwa heels ndefu zinaweza kuchangia matatizo kama maumivu ya sehemu ya mbele ya mguu na kuongeza hatari ya kuumia kifundo.


MUDA WA KUVAA HEELS

Hakuna idadi maalumu ya saa inayofaa kwa kila mtu, kwa sababu afya ya mguu, aina ya kiatu, urefu wa kisigino na shughuli unayofanya hutofautiana.

Hata hivyo, kanuni rahisi ni kutotumia heels ndefu kwa muda mrefu, hasa kama unajua utasimama au kutembea kwa muda mrefu.

Daktari Israel Natse anashauri, “Usifanye heels ndefu kuwa kiatu cha siku nzima kama kazi yako inakulazimisha kutembea au kusimama muda mrefu.

Kwa matumizi ya kawaida, kisigino kifupi na chenye uimara husaidia kupunguza mzigo kwenye sehemu ya mbele ya mguu.”

KWA SHEREHE, KAZI AU KUTEMBEA?

Heels ndefu zinaweza kutumika zaidi kwenye hafla ambazo mtu hatatembea sana, kama sherehe, chakula cha jioni au tukio maalumu.

Lakini kama unaenda safari ya kutembea, kufanya manunuzi, kusimama muda mrefu au kutumia siku nzima nje, ni bora kuchagua kiatu kifupi, chenye nafasi ya kutosha kwa vidole na kinachoshikilia mguu vizuri.

Utafiti uliofanywa na Harvard Health inaeleza kuwa kiatu kinachofaa kinapaswa kuwa na nafasi ya kutosha kwenye vidole, kisibane mguu na kiwe na uwezo mzuri wa kupunguza mshtuko wakati wa kutembea.


MAGOTI, MGONGO NA MKAO

Heels hazibani miguu pekee. Kisigino kikiwa juu, uzito wa mwili unasogezwa mbele na mkao wa mwili hubadilika. Harvard Health inaeleza kuwa heels ndefu zinaweza kuhusishwa na maumivu ya mgongo, mabadiliko ya mkao na kufupika kwa misuli ya ndama.

Daktari Israel anaonya, “Tatizo si uzuri wa heels wenyewe, bali matumizi yake ya mara kwa mara na kwa muda mrefu. Mwili unapolazimika kubeba uzito katika mkao usio wa kawaida, miguu na sehemu nyingine za mwili zinaweza kuanza kuonyesha maumivu.”

VIDOLE NAVYO VINALIA

Heels zikiwa pamoja na sehemu ya mbele ya kiatu iliyo finyu, vidole husukumwa kuelekea mbele.

Hali hiyo inaweza kuchangia matatizo kama vidole kujikunja, malengelenge, ngozi ngumu na kuongezeka kwa tatizo la kidole gumba kupinda upande.

Harvard inaeleza kuwa matumizi ya viatu vyenye kubana na heels kwa muda mrefu ni miongoni mwa mambo yanayochangia tatizo la vidole kujikunja.