Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Freiburg ilivyokwea kileleni, Isco akiendeleza moto Betis

TAKWIMU Pict

Muktasari:

  • Kwa ushindi huo Freiburg, ambayo tayari ilikuwa imeweka rekodi mpya ya klabu kwa kuanza msimu vizuri zaidi baada ya kukusanya pointi 10 katika mechi nne za mwanzo, ilifikisha pointi 13 na kuongoza kwa tofauti ya mabao dhidi ya Borussia Dortmund. Mabingwa watetezi, Bayern Munich, waliotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Augsburg, Jumamosi, wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 11.

DORTMUND, UJERUMANI: FREIBURG, ikiwa na wachezaji 10 uwanjani ilipata bao la ushindi dakika ya 85 kupitia mshambuliaji wa kiamtaifa wa Japan, Keisuke Goto na kuichapa Schalke 04 kwa mabao 2-1 nyumbani, matokeo yaliyoipandisha kileleni mwa Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga).

Kwa ushindi huo Freiburg, ambayo tayari ilikuwa imeweka rekodi mpya ya klabu kwa kuanza msimu vizuri zaidi baada ya kukusanya pointi 10 katika mechi nne za mwanzo, ilifikisha pointi 13 na kuongoza kwa tofauti ya mabao dhidi ya Borussia Dortmund. Mabingwa watetezi, Bayern Munich, waliotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Augsburg, Jumamosi, wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 11.

Freiburg, iliyotawala mchezo ilitangulia kupata bao dakika ya 10 kupitia kiungo Maximilian Eggestein, lakini Schalke ilisawazisha katika dakika ya 30 kupitia beki wa kulia Adrian Gantenbein. Katika kipindi cha pili Freiburg ilipungukiwa mchezaji mmoja kwenye dakika ya 64 baada ya winga wa Kijapani Yuito Suzuki kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, hali iliyotarajiwa kuipa Schalke nafasi ya kutawala mchezo.

Hata hivyo, wageni walicheza kwa tahadhari kupita kiasi na kukosa makali katika mashambulizi kiasi cha kushindwa kutumia faida ya kuwa na mchezaji mmoja zaidi. Freiburg iliwaadhibu dakika tano kabla ya mchezo kumalizika, wakati Goto  alipofunga bao la ushindi kwa kichwa kilichogusa mpira na kuubadili mwelekeo ukajaa nyavuni.


TAKWI 03

GLADBACH MATESO

Katika kipute kingine cha ligi hiyo kilishuhudia Borussia Monchengladbach maarufu kama Gladbach ikiendelea kubaki mkiani mwa Bundesliga baada ya kufungwa mabao 2-1 na wapinzani wao wa karibu, Cologne katika mchezo uliofunikwa na vurugu zilizotokea kwenye majukwaa ya mashabiki.

Mchezo ulisimamishwa kwa dakika kadhaa huku polisi wa kutuliza ghasia wakilizunguka eneo la mashabiki wa timu ngeni, baada ya mashabiki wa Gladbach kuonekana kurusha fataki kuelekea upande wa mashabiki wenyeji kufuatia bao la pili la Cologne lililofungwa kwa ustadi na Said El Mala katika kipindi cha pili.

Matokeo hayo yaliendeleza mwanzo mbaya wa Gladbach, ambayo bado haijapata pointi yoyote msimu huu. Kocha mpya, Alexander Blessin, alishindwa kuizuia timu hiyo kupoteza mchezo wake wa tano mfululizo katika mechi tano za mwanzo za msimu.


TAKWI 02

ISCO AIPAISHA BETIS LALIGA

Ukiachana na Bundesliga, katika Ligi Kuu Hispania (La Liga), kiungo mshambuliaji wa Real Betis, Francisco Roman Alarcon Suarez maarufu Isco alifunga bao katika kila kipindi wakati timu yake ilipopata ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Osasuna nyumbani na kupanda hadi nafasi ya tatu katika La Liga. Betis sasa iko pointi tano nyuma ya vinara Barcelona na moja mbele ya Real Madrid.

Isco alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 10 kwa kufunga penalti, kabla ya Abde Ezzalzouli kuongeza bao la pili kabla ya mapumziko baada ya Betis kuupokonya mpira kwa wapinzani wao katika eneo la juu la uwanja na kufanya shambulizi la kushtukiza kwa kasi.

Betis ilionekana kuwa katika nafasi nzuri ya kupata ushindi rahisi baada ya Diego Llorente kufunga bao la tatu dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Hata hivyo, Osasuna ilifunga mabao mawili ya haraka kupitia Ante Budimir na Raul García, na kupunguza tofauti ya mabao hadi 3-2 dakika ya 56.

Baada ya hapo Isco aliendeleza moto alipouwahi mpira uliokuwa ukizagaa ndani ya eneo la hatari la wapinzani wao na kupiga shuti lililojaa wavuni. Kana kwamba haitoshi, Jose Antonio Morante, aliyeingia akitokea benchi, alifunga bao lingine katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90, na kuifanya Betis kufikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi nane.

Mapema kabla ya mchezo huo Real Sociedad ilipambana dhidi ya Deportivo La Coruna kurejea mchezoni na kupata ushindi wa mabao 3-2 nyumbani, huku Elche, inayolazimika kupambana ikipata pointi muhimu baada ya kutoka suluhu dhidi ya Celta Vigo iliyokuwa ugenini.


TAKWI 04

LAZIO YAIFIKIA INTER

Lazio ilifikisha pointi sawa na Inter Milan iliyopo kileleni mwa msimao wa Ligi Kuu Italia (Serie A) baada ya kuichapa Monza kwa mabao 3-1 Jumapili, ushindi ulioifanya kuishusha Roma hadi nafasi ya tatu.

Lazio imefikisha pointi 16 baada ya ushindi mara tano na sare moja, huku ikizidiwa na Inter Milan kwa mabao ya kufunga ikiwa nayo 11 dhidi ya 18 ya mabingwa hao watetezi wa Serie A.

Nayo Roma ikiwa na wachezaji 10 uwanjani ilitoka suluhu na Como katika mchezo uliokuwa wa kwanza msimu huu wa Serie A kumalizika bila kufungana.