Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fahamu chanzo cha mashindano ya kula Marekani

KULA Pict

Muktasari:

  • Leo tumekusogezea undani wake, kuanzia jinsi unavyochezwa, kanuni, zawadi na kila kitu kinachohusiana na mashindano ya kula misosi.

NEW YORK, MAREKANI: WAKATI wewe unakula ili upoze njaa, kuna watu wengine muda huu wapo bize kufanya kazi yao ambayo ni kula. Ndio, inawezekana umeshuhudia mechi nyingi za mpira wa miguu na michezo mingine, lakini maajabu hayaishi duniani na huu hapa ni kati ya michezo ambayo haina umaarufu sana duniani, ila umekuwa ukichezwa sehemu mbalimbali na kuna mastaa kabisa waliotengeneza majina kutokana na uwezo wao wa kufakamia misosi.

Leo tumekusogezea undani wake, kuanzia jinsi unavyochezwa, kanuni, zawadi na kila kitu kinachohusiana na mashindano ya kula misosi.

KUL 01

ASILI YAKE

Mashindano ya kula ni mchezo wa kipekee ambao umepata umaarufu mkubwa katika karne ya 20 na 21. Historia inaonyesha mchezo huu asili yake ni Marekani, ingawa mila ya watu kushindana kula ilikuwepo tangu zamani katika baadhi ya jamii licha ya kwamba hayakuwa mashindano rasmi yaliyotambulika.

Mchezo huu ulianzia huko Coney Island, New York, katika mgahawa wa Nathan’s Famous mwaka 1910 na ilipofika Juni 4, 1916 ulijipatia umaarufu zaidi na watu wengi wakawa wanaenda kuutazama.

Kwa muda huo mashindano yalikuwa yanafanyika katika mgahawa wa Nathan’s Famous pekee, lakini taratibu sehemu nyingine pia zikawa zinaanzisha mashindano mengine.

Kufikia mwaka 1990, Shirikisho maalumu la kusimamia michezo hii lilianzishwa huko Marekani na likaitwa Major League Eating (MLE) ambapo washindani wote kutoka sehemu mbalimbali za dunia husajiliwa, pia kuna viwango vya ubora ambavyo hubadilika kulingana na rekodi za washindani.

Mwaka 2000, televisheni zilianza kurusha rasmi mashindano haya na ikasaidia kuyaongezea umaarufu zaidi duniani.

KUL 02

SHERIA ZA MASHINDANO

Sheria hutegemea na aina ya chakula kinacholiwa katika mashindano husika, lakini kwa ujumla katika suala la muda huchukua kati ya dakika nane hadi 10 kwa mashindano makubwa na kuna mashindano madogo ambayo hutumia dakika tano tu.

Kula Sahihi: Chakula kinachohesabiwa ni kile ambacho kimeshamezwa kikamilifu baada ya muda wa shindano kuisha, kile kilichobaki mdomoni hakihesabiwi na vina jina lake la utani la 'chipmunking'.

Vilevile mchezaji akionekana anatapika wakati wa kula, huondolewa katika shindano mara moja na mwenzake kupewa ushindi.

Hairuhusiwi mchezaji husika kutumia kijiko au kifaa kingine bali anatakiwa kula kupitia mkono wake, isipokuwa kwa vyakula ambavyo haiwezekano kula kwa mkono.

Wachezaji wakikutwa na kosa la udanganyifu kama kuficha chakula au kutupa chini hufutwa na wakati mwingine hufungiwa na shirikisho la MLE.

Washiriki huruhusiwa kutumia maji, maziwa, soda au juisi ili kusaidia kumeza chakula haraka.

Chakula kinaweza kugawanywa vipande vidogo au kulowekwa kwenye maji kabla ya kumezwa, ilimradi kisibadilishwe kabisa kuwa supu.

Usalama: Daktari au wahudumu wa afya lazima wawe karibu muda wote wa shindano,

washiriki wote hulazimika kusaini fomu ya kiapo cha kukubali kushiriki na hata ikitokea bahati mbaya wamepata madhara basi hakutokuwa na kushtaki.

Mashindano hayaruhusiwi kushiriki kwa watu wenye matatizo ya kiafya yanayohusiana na tumbo au koo.

KUL 03

VIGEZO VYA WASHIRIKI

Washiriki lazima wawe na umri wa miaka 18 au zaidi na kwa mashindano ya kimataifa wa lazima wawe wamesajiliwa na MLE.

Katika mashindano makubwa, wachezaji hupitia katika mchujo kabla ya kushiriki katika shindano la mwisho ambalo ndio kubwa zaidi duniani na hili mara nyingi huandaliwa na MLE wenyewe.

Kila mchezaji huwa na mwamuzi wake anayehesabu idadi ya chakula kilicholiwa na namna wanavyohesabu ni huwa wanapima kutumia vipimo sahihi kama ni kilo, gramu au kama ni chakula ambacho hakihitaji kupimwa huwa wanahesabu vipande vilivyobakia.

Mchezo huu ambao huwa na washiriki wasiopungua watano, endapo wawili kati yao wanamaliza kwa idadi sawa ya vyakula, mzunguko wa ziada huongezwa ili kumpata mshindi na mara nyingi hupewa dakika mbili ya kumaliza sahani yenye chakula kidogo.

KUL 04

ZAWADI

Zawadi zinatofautiana kulingana na mashindano husika. Mashindano makubwa kama Nathan’s Famous Hot Dog Eating Contest, washindi hupata hadi Dola 10,000 (takriban Sh26 milioni) na mkanda wa ubingwa.

Mashindano madogo huwa na zawadi ndogo zaidi, mara nyingi ni pesa taslimu, vyeti au ufadhili kutoka kwa kampuni za vyakula.

Baadhi ya wachezaji wakubwa hupata udhamini na mikataba ya matangazo kutoka kwa kampuni hizo.

KUL 05

UNAKOCHEZWA ZAIDI

Mchezo huu huchezwa sana Marekani ambako ndio kama kitovu cha mashindano haya na pia ndipo yalipo makao makuu ya MLE.

Vilevile Japan mchezo huu huchezwa sana huku nchi hiyo ikizalisha mastaa wakubwa kama Takeru Kobayashi Kobayashi, ambaye anasumbua sana katika mashindano ya dunia.

Canada na Uingereza pia zina mashindano ya vyakula vya kienyeji kama burger kubwa na samaki, pia Australia nayo inacheza mchezo huu na hivi karibuni iliripotiwa kuomba uenyeji wa mashindano ya kimataifa.

KUL 06

MASHINDANO YAKE

Nathan’s Famous Hot Dog Eating Contest - Coney Island, New York (Marekani)

Hufanyika kila tarehe 4 Julai, siku ya Uhuru wa Marekani.

World Chicken Wing Eating Championship -Buffalo, New York (Mashindano ya kula vipapatio vya kuku)

World Burrito Eating Championship - New Mexico (Marekani)

World Pizza Eating Championship - California (Marekani)

World Ice Cream Eating Championship - Florida (Marekani)

World Donut Eating Championship - Texas, (Marekani)

World Oyster Eating Championship - New Orleans, Louisiana

World Taco Eating Championship -Las Vegas, Nevada (Marekani)

Ribs Eating Championship - Chicago, Illinois (Marekani)

Kale Eating Championship - California (Marekani)

KUL 07

VYAKULA VINAVYOLIWA

Mbali na hot dogs, MLE inasimamia mashindano ya vyakula mbalimbali kama:

Burger kubwa

Pizza

Vipapatio vya kuku

Ice cream

Tacos

Donuts

Tambi


CHANGAMOTO

Licha ya kuwa burudani, mchezo huu umekosolewa kwa sababu:

Unaweza kusababisha athari za kiafya kama vile kumeza vibaya, matatizo ya tumbo, au kushindwa kupumua.

Unapingana na kampeni za kupunguza upotevu wa chakula hasa katika nchi zenye uhaba wa chakula.


MABINGWA

Joey Chestnut wa Marekani ndiye mshindi mara nyingi wa Nathan’s Hot Dog Eating Contest; anashikilia rekodi ya kula hot dogs 76 ndani ya dakika 10 (2021).

Takeru Kobayashi (Japan) - Huyu ni nyota wa kwanza wa kimataifa wa mashindano haya ambaye alishinda mashindano yaliyofanyika Marekani akitokea Japan.

Miki Sudo (Marekani) - Anatajwa kuwa ni mwanamke bora zaidi kwenye historia ya mchezo huu.