Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Europa ligi iitwe unai Emery Cup

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Liliitwa hivyo kwa heshima ya Rais wa tatu wa FIFA, Jules Rimet, Mfaransa aliyeliongoza shirikisho hilo kwa miaka 33, kuanzia mwaka 1921 hadi 1954.

Kombe la Dunia la zamani, kabla ya hili la sasa la FIFA, liliitwa Jules Rimet Cup yaani Kombe la Jules Rimet.

Liliitwa hivyo kwa heshima ya Rais wa tatu wa FIFA, Jules Rimet, Mfaransa aliyeliongoza shirikisho hilo kwa miaka 33, kuanzia mwaka 1921 hadi 1954.

Kwa muda huu wa uongozi wake, anabaki kuwa kiongozi wa FIFA aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi kihistoria.

Katika utawala wake ndio mashindano ya Kombe la Dunia yalianza, mwaka 1930.

Kutokana na mchango wake katika kuanzishwa kwa mashindano hayo, lile Kombe ambalo bingwa anapewa, likaitwa kwa jina lake, Jules Rimet Cup.

Jina hili liliendelea hadi mwaka 1970 pale Brazil na Pele wao walipotwaa ubingwa kwa mara ya tatu, na kupewa kombe moja kwa moja.

PUMZ 01

Ndipo likaletwa Kombe jipya lililoitwa Kombe la Dunia la FIFA yaani FIFA World Cup, ambalo Argentina na Messi wao wanalishikilia kama mabingwa watetezi.

Heshima aliyopewa Jules Rimet ndio anayostahili kocha wa Aston Villa, Unai Emery, raia wa Hispania, kwenye Kombe la Europa Ligi. Unai Emery ndio kocha mwenye mafanikio makubwa zaidi kwenye historia ya mashindano ya Kombe UEFA na Europa Ligi. Ametwaa ubingwa mara tano akiwa na klabu tatu tofauti.


Aston Villa (2025/26):

Baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Freiburg ya Ujerumani, kwenye fainali iliyochezwa huko Istanbul, Uturuki.


Villarreal (2020/21):

Baada ya kuwafunga Manchester United kwa mikwaju 11-10 ya penati kufuatia sare ya 1-1 dakika 120. Fainali hii ilifanyika mjini Gdansk huko Poland.


Sevilla (2015/16):

Baada ya kuwafunga Liverpool 3-1 kwenye fainali iliyofanyika Basel, Uswisi.


Sevilla (2014/15):

Baada ya kuwafunga 3-2 Dnipro kutoka Ukraine, kwenye fainali iliyofanyika Warsaw, Poland

PUMZ 02

Sevilla (2013/14):

Baada ya kuwafunga Benfica 4-2 kutoka Ureno, kwenye fainali iliyofanyika Turin, Italia.

Emery pia aliiongoza Arsenal kucheza fainali ya Europa Ligi mwaka 2019 waliyopoteza kwa Chelsea.

Kwa jumla, anashikilia rekodi ya mashindano hayo kwa kucheza mechi nyingi zaidi, kushinda mechi nyingi zaidi na fainali nyingi zaidi.

Ama kwa hakika Unai Emery ni mfalme asiye na kifani (Undisputed King) wa mashindano haya, kuanzia zama za UEFA Cup hadi sasa Europa Ligi.

Kutokana na hilo, anastahili kabisa kupewa heshima ya aina yake, ikiwemo kuyaita mashindano haya kwa jina lake.

Ni kama ambavyo tuzo ya kipa bora wa dunia inaitwa Yashin, ni kwa heshima ya Lev Yashin, kipa wa zamani wa Urusi, kipa wa kwanza pekee hadi sasa kuwahi kushinda Ballon d’Or (1963).

PUMZ 03

Katika wakati wake wa kucheza, aliokoa jumla ya penati 150...

Hata tuzo ya goli bora la dunia inaitwa Puskas, ni kwa heshima ya Ferenc Puskas, straika la mabao la Hungary na Real Madrid miaka ya 1950.

Katika ubora wake Puskas alikuwa moto wa kuotea mbali kwa kufunga, sio tu magoli mengi bali magoli mazuri.

Puskas alifunga jumla ya mabao 806 kwenye mechi rasmu 793.

Alikuwa anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwa timu za taifa, kwa mabao yake 84 kwenye mechi 85 akiwa na timu yake ya taifa ya Hungary. Orodha ni ndefu ya majina ya watu waliofanya mambo makubwa hadi kupewa majina yao kwenye soka.

Lakini kubwa kuliko yote ni RUGBY. Bila shaka umeshasikia jina hili, au tuseme mchezo huu.

Kiasi RUGBY au RAGGA kwa jina la utani, ni mchezo wa mpira wa miguu. Na ndio maana nchini Marekani mchezo huu unaitwa Football...japo sheria zake zinatofautiana kidogo.

Ni hivi, wengi hudhani mchezo huu tunaoupenda (mpira wa miguu) unaitwa hivyo kwa sababu unachezwa zaidi kwa kutumia miguu...la hasha.

Unaitwa mpira wa miguu kwa sababu nyingine kabisa, nje ya namna ya kuucheza.

Mchezo huu ulipoanza, hakukuwa na sheria ya kuwadhibiti wachezaji hivyo walitumia kila kiungo walichoona kitawasaidia.

Kwa kuwa hakukuwa na sheria, kila timu ilitumia mpira iliokuwa nao...hakukuwa na kipimo cha ukubwa wa mpira. Hii ikaleta shida pale kila timu ilipokuja na mpira wake wa ukubwa tofauti.

PUMZ 04

Kumaliza tatizo hilo, ukapimwa miguu wa mfalme wa Uingereza, na urefu wa miguu huo (pale pa kuvalia vitatu yaani foot) ndio kiwa kipenyo cha ukubwa wa mpira. Kwa kuwa walipima mguu (foot), ndio mchezo ukaitwa mpira wa miguu...lakini kuucheza kulihusisha kila kiungo, zaidi mikono.

Hali hiyo iliendelea hadi 1863 pale sheria rasmi za mchezo huu zilipotungwa na kukataza matumizi ya mikono. Pia kikaundwa chama rasmi cha kusimamia sheria hizi, kikaitwa chama cha mpira, Football Association...ndio hicho cha Uingereza hadi sasa.

Kuna baadhi ya timu zilizokuwepo wakati huo zikapinga kuacha kutumia mikono. Kwa hiyo timu hizo zikaendelea kucheza mpira wa miguu kwa kutumia zaidi mikono.

Zika kataa kuwa chini ya Football Association, zikaanzisha chama chao walichokiita Football Union.

Kwa hiyo kukawa na vyama viwili vya Football; kimoja cha Football isiyoruhusu matumizi ya mikono, Football Association, na kingine cha Football inayoruhusu matumizi ya mikono, Football Union.

Kila chama kikasimamia mchezo wake, na mchezo huo ukaitwa jina la chama hicho.

Ile football iliyosimamiwa na Football Association, ukaitwa Association Football.

Na ile football iliyosimamiwa na Football Union ikaitwa Union Football.

Na hii ineendelea hadi leo, mpira wa miguu jina lake rasmi ni Association Football...sio tu Football. Baadaye kila chama kikaanzisha ligi yake ikitumia jina la mchezo wake kinaousimamia. Kukawa na Association Football League na Union Football League.

Ile ligi ya Football Union, inayoruhusu matumizi ya mikono, ikatawaliwa na shule moja iliyoitwa Rugby. Timu ya shule hii ikawa inashinda ubingwa kila msimu kiasi kwamba mchezo ule ukaonekana kama wao kwao...na ndipo jina la mchezo ule likawa RUGBY

Kwa hiyo jina la RUGBY ni kwa heshima ya timu ya shule ya RUGBY.

Kwanini Unai Emery ambaye amekuwa akishinda ubingwa wa Europa asipewe heshima yake?