Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAUAJI YA KUTISHA -17

Muktasari:

  • Akajua kuwa bosi wake alikuwa anampigia baada ya kupata taarifa ya mauaji ya mtoto mwingine wa Almasi.

UTANGULIZI

Aliporudi tena ofisini kwake simu yake  ikaita.  Alipotazama  namba inayompigia akaona namba za Mkurugenzi wa Upelelezi.

Akajua kuwa bosi wake alikuwa anampigia baada ya kupata taarifa ya mauaji ya mtoto mwingine wa Almasi.

Siku chache tu zilizopita, Amour alimwambia bosi wake huyo kuwa aliwakamata watu waliokuwa  wakiwaua  watoto  wa Almasi na bosi huyo aliamini kuwa tatizo hilo lilikuwa limekwisha.


SASA ENDELEA...


Sasa atamueleza nini kuhusu mauaji yaliyotokea?

Amour alitaka asiipokee simu lakini hakuweza kuiacha simu ya bosi wake bila kuipokea. Akaipokea huku akiwa hajui ataambiwa nini.

“Amour unachelewa kupokea simu!” Sauti ya mkurugenzi ikasikika kwenye simu.

“Afande ndio nimeingia ofisini na kukuta simu inaita.” Amour alijihami.

“Siku ile ulinieleza nini na hii leo nini kimetokea?”

“Nadhani unakusudia kuhusu kijana aliyeuawa Mto Wami?”

“Ndiyo.”

“Siku ile tulikamata majambazi ambao tuliamini kabisa ndio waliokuwa wanahusika na mauaji ya familia ya Almasi. Lakini leo tena kuna kijana wake mwingine ameuawa. Sijajua ni kina nani waliomuua na ni kwa sababu gani?”

“Kwanini umechelewa kunipa taarifa?’

“Ndiyo nilikuwa nakuja ofisini nikupigie.”

“Muda wote ulikuwa unafanya nini?’

“Nilikwenda Chalinze. Niliporudi nilikwenda hospitali ya Muhimbili. Nilipotoka huko nilimuita Almasi na kumpa taarifa ya mauaji ya mwanawe na nilimpeleka Muhimbili kuuona mwili wa mwanawe. Sasa ndio nimerudi ofisini.”

“Amour maelezo niliyoyapata ni kwamba watu waliomuua huyu kijana ni wale wale waliowaua watoto wengine wa Almasi!”

“Hili suala linahitaji uchunguzi. Nasubiri nipate maelezo ya polisi wawili wa Handeni walioshuhudia hilo tukio”

“Hao polisi wako wapi?”

“Wako Handeni. Walishuhudia hilo tukio wakati wanatoka Dar wakielekea Handeni wakisindikiza gari la benki lililokuwa na pesa.”

“Wao walishuhudia wakati kijana huyo akiuawa?’

“Ndiyo afande.”

“Walichukua hatua  gani?”

“Walimueleza mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze kuwa waliposimamisha gari, watu hao walitoweka ghafla na hawakuwahi kuchukua hatua yoyote.”

“Kwa hiyo wao wamewaona hao majambazi?”

“Wamewaona wakiwa kwenye gari  na ndio waliowapigia simu polisi wa Chalinze.”

“Utakutana nao lini?”

“Kesho watakuja ama hapa Dar au Chalinze kutoa maelezo yao.”

“Kama itabainika kuwa wauaji walikuwa ni wale wale utakubali kwamba hao uliowakamata hawakuhusika  na mauaji hayo?”

“Afande siwezi kuwa na jibu kwa sasa ila ni mpaka hapo nitakapopata maelezo kwa hao polisi hapo kesho.”

“Kitu kingine ambacho ninakuonya, usipende kukimbilia kueleza kuwa umemaliza tatizo kabla ya kuhakikisha kuwa hilo tatizo umelimaliza kweli. Wakati mwingine utajikuta unashindwa kujibu maswali na kulitia aibu jeshi la polisi.”

“Ni kweli afande. Nilifanya kosa.” Amour alikubali yaishe.

Mkurugenzi akakata simu.

Amour alitoa kitambaa kutoka mfukoni mwake akakikunjua na kujifuta chembe za jasho zilizokuwa zimetanda usoni kwake kisha akakikunja tena na kukirudisha mfukoni. Alijua ni kwa nini alitoka jasho. Alitoka jasho kwa sababu alilazimika  kuzuia hamaki iliyokuwa inampanda wakati akizungumza na bosi wake.

Suala la bosi huyo kumwambia kuwa alikosea kueleza kuwa alikuwa amewakamata wauaji wa familia ya Almasi lilimkera. Lilimkera kwa sababu aliona mkurugenzi wake alikuwa amemdharau kumwambia hivyo.

Alikaa ofisini hapo hadi alipoona imetimia saa kumi jioni akaondoka.

Huko nyumbani kwa Almasi nako hakukuwa shwari. Almasi alipofika nyumbani kwake na kumueleza mke wake kilichompata mtoto wao, alianguka mwenyewe na kupotewa na fahamu.

Mke wake aliwapigia simu  watoto wao wawili waliobaki Alex na Benjamin ambao walifika dakika  chache tu baada ya Almasi kuanguka.

Alex na Benjamin walipomuona baba yao akiwa hajitambui walimbeba wakampakia kwenye gari na kumpeleka hospitali. Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa presha ilikuwa imepanda sana. Almasi alilazwa na kuwekewa dripu.

Alex alibaki na baba yake, Benjamin akarudi nyumbani. Hawakujua washughulikie kipi, msiba wa John au ugonjwa wa Almasi!

Baada ya kuwaarifu ndugu  na  jamaa ndipo masuala yote mawili yalipoanza kushughulikiwa.

Mwili wa  John ulichukuliwa hospitali saa tano ya siku iliyofuata. Uliletwa nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Almasi alikuwa amezinduka tangu usiku uliopita na hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri lakini ilipofika saa nne akataka aruhusiwe aende akamzike mtoto wake.

Mwanawe Alex alikuwepo karibu, akaenda kumuita daktari.

“Daktari najiona niko vizuri naomba uniruhusu nikamzike mwanangu.”

Almasi alimwambia daktari wake alipokwenda kumsikiliza.

“Sipendekezi uondoke hospitalini kwa sababu bado unahitajika kuwa kwenye mapumziko.” Dakatari alimwambia.

“Kusema kweli najisikia vizuri na ninahitajika kumzika mwanangu aliyeuawa jana.”

“Ni sawa lakini mimi sipendekezi uondoke kwa sasa.”

“Yaani dokta unanizuia nisimzike mwanangu?”

“Sikuzii, ni hali yako bado haijaridhisha.”

“Baba ungemsikiliza dakatari anavyokwambia.” Alex akamwambia baba yake.

“Sitamsikiliza. Nahitaji kwenda kumzika  mtoto wangu. Hata wewe unatakiwa kwenda kumzika kaka yako.”

Almasi aliamua kuondoka mwenyewe hapo hospitali bila kuruhusiwa  na dakatari wake, akapakiwa na Alex kwenye gari na kurudishwa nyumbani.

Alikuta maandalizi ya mazishi yalikuwa yakiendelea. Mpaka saa kumi jioni, mwili wa John ulipelekwa kuzikwa.

Almasi alichanganyikiwa hata kumteua mtoto wake mwingine kushika nafasi ya John. Akaamua kuiacha wazi nafasi hiyo kwa muda.

Ilikuwa ni saa saba ya siku aliyozikwa John ambapo Amour alipigiwa simu kutoka Chalinze na kujulishwa kuwa wale polisi wawili walikuwa wamefika.

“Imeamuliwa kwamba waje huku Dar. Wapande basi waje huku.” Amour alimwambia mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze aliyekuwa amempigia simu.

“Kwa hiyo tusichukue maelezo yao?”

“Msichukue. Kuna mambo muhimu ambayo tunataka kuyajua.”

“Sawa. Sasa  ninawaagiza wapande basi waje huko.”

“Muda wowote watakapofika waje moja  kwa  moja ofisini kwangu.”

“Nitawaagiza wafike moja kwa moja ofisini kwako.”

“Sawa.”

Saa tisa alasiri polisi hao wakafika jijini Dar. Walikwenda moja kwa moja ofisini kwa Inspekta Amour.

Baada ya kupeana salamu za kipolisi na Inspekta Amour, polisi hao walikaa kwenye viti. Amour alikuwa ameshaandaa karatasi  kwa ajili ya kuchukua maelezo yao.

Aliwaandika majina yao na namba zao za kipolisi pamoja na vituo vyao vya kazi.

“Nitakuwa ninamhoji mmoja mmoja lakini anaposahau kitu mwenzake anaweza kumkumbusha.”  Amour aliwambia.

Polisi aliyemuhoji kwanza jina lake lilikuwa Deo.

“Nimeambiwa kwamba jana mlikuwa katika gari ya benki mkitokea Dar kuelekea Handeni. Ni kwelli?” Amor akamuuliza Deo.

“Ni kweli. Tulikuwa tukisindikiza pesa za benki.”

“Mlikuwa polisi wawili,  wewe  na mwenzako?”

“Ndiyo tulikuwa wawili.”

“Ndani ya hilo gari mlikuwa na maafisa wangapi wa benki?”

“Kulikuwa na maafisa wawili.”

“Jumla mlikuwa watu wanne?”

“Ni watano pamoja na dereva.”

“Sawa. Sasa hebu nieleze kama ni kweli mlishuhudia tukio la mauaji baada ya kuvuka daraja la Mto Wami?”

“Ni kweli.”

“Sasa  nataka unieleze ulichokishuhudia.”

“Sawa. Wakati tunamaliza kuvuka daraja la Mto Wami tuliona gari iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa barabara. Tuliona mtu mmoja kama alikuwa anabadili tairi moja la nyuma baada ya kupata panchari.”

“Ndiyo…”

“Lakini ghafla tukaona watu watatu wametokea na kumzunguka yule mtu aliyekuwa anabadili tairi.”

“Hao watu walitokea kwa wapi?”

“Nafikiri walitokea kwenye msitu.”

“Nataka hapo penye hao watu watatu. Hebu nieleze vizuri hao watu walikuwaje na walikuwa wamevaa nini?”

“Walivaa mavazi ya ajabu kidogo. Wawili walivaa mavazi meupe. Mmoja alivaa mavazi meusi.”

“Walikuwaje?’

“Labda tofauti ilikuwa kwa yule aliyemchinja marehemu. Yeye mwenyewe shingo yake ilionekana kama imechinjwa. Kichwa chake kilikuwa kama kinataka kuanguka

Amour alipoyasikia maelezo hayo alikunja uso akaduwaa kidogo. Kimoyomoyo alikuwa akijiambia watu hao ndio wale wale aliokuwa akiwatafuta. Aliamini moja kwa moja kwamba majambazi waliowakamata na wengine kuwaua hawakuhusika.

“Hii  ni aibu kwa jeshi la polisi,” alijiambia kimoyo  mmoyo.

“Hawa watu wanatumia uchawi wa aina gani kuzuia  wasikamatwe?” Akaendelea kujiuliza.

“Baada ya mtu huyo kumchinja marehemu walifanya nini?” Amour akaendelea kumuuliza maswali yule polisi.

“Ndio wakati  ule tunasimamisha gari. Gari liliposimama tuliwania kutoka ili tuwakamate wale watu lakini hatukuwaona tena.”

“Ni kwanini hamkuwaona wakati walikuwapo mahali hapo?”

“Bila shaka walipotuona tunasimamisha gari walikimbilia msituni. Msitu ulikuwa karibu sana.”

“Una  uhakika kwamba walikimbilia msituni?”

Yule polisi aliyeulizwa alimtazama polisi mwenzake.

“Itakuwa wamekimbilia msituni.” Polisi aliyetazamwa na mwenzake alijibu bila kuulizwa.

“Hamkuweza kuwafuatilia?”

“Hatukujua walikimbilia upande gani. Isitoshe tulikuwa na jukumu jingine la kulinda zile pesa. Tusingeweza kuziacha  na kuingia msituni kuwatafuta.”