Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Phina na urembo, ushikaji na Eni utaupenda!

PHINA Pict

Muktasari:

  • Mwanaspoti limefanya mahojiano na Phina kwa simu kutokana na kutokuwepo nchini, na hapa anazungumzia ukaribu wake na Eni, alichozungumza na mwanamuziki nguli Bob Rudala na jinsi anavyoiona kazi yake kimataifa.

MSANII Bongo Fleva, Sarah Michael 'Phina' amekuwa akifuatiliwa zaidi katika mitandao ya kijamii kutokana na ukaribu wake na supastaa kutoka nchini Nigeria Eni Adeoluwa ambaye ni muigizaji, msanii wa muziki na mtengeneza maudhui (content creator).

Mwanaspoti limefanya mahojiano na Phina kwa simu kutokana na kutokuwepo nchini, na hapa anazungumzia ukaribu wake na Eni, alichozungumza na mwanamuziki nguli Bob Rudala na jinsi anavyoiona kazi yake kimataifa.

PHIN 01

JUX KATIKATI YA PHINA NA ENI

Anasimulia mwanzo wa safari wa urafiki wao baina yake na Eni, ilianzia katika harusi ya msanii wa bongo fleva, Juma Jux na mkewe Priscilla, wakaanza kwa kusalimiana kubadilishana na kualikana kula pamoja chakula.

"Japokuwa nilikuwa nilikuwa namfuatilia katika mitandao ya kijamii kama Instagram pia yeye alikuwa anafanya hivyo, baada ya kukutana katika harusi hiyo ikwa rahisi kufanya kazi pamoja," anasema Phina na kuongeza;

"Eni ndiye aliyetoa wazo la kufanya kazi pamoja, mfano tulianza baada ya kunialika chakula na anafuatiliwa zaidi katika mitandao ya kijamii kutokana na kontenti za vyakula, kisha tukafanya kava ya wimbo wa taifa la Tanzania pia ukapokelewa kwa ukubwa zaidi.

"Lengo la kuimba naye wimbo huo ilikuwa ni kukitangaza Kiswahili baada ya hapo tukafanya vitu vingi mbalimbali na ana mchango mkubwa wa kuendelea kujifunza kujua levo za kimataifa zinataka kitu gani."

Mbali na wimbo wa Taifa wa Tanzania, Phina amefanya kava za  nyimbo za wasanii wengine na Eni kama Smile For Me, Nimekuchagua Wewe ya msanii mkongwe Bob Rudala kutokana na ukaribu wao huo wengi wao wamekuwa wakihisi kama wapo katika mahusiano.

Anaelezea ukaribu wao akisema: "Sisi ni washikaji na vaibu zetu zinaendana, kanifungulia koneksheni ya kufanya kazi na soko la watu wengine waliyoongezeka nje na Tanzania, hivyo kikubwa nawashukuru mashabiki kwa kutupokea na kutuona pamoja."

Anasema bado wana kazi nyingi ambazo bado hawajaziachia pia anajifunza uwekezaji katika muziki ili kufikia levo ya ushindani wa kimataifa.

"Muziki wa kimataifa kuna uwekezaji mkubwa wa pesa,muda, kujifunza vitu vipya nimeanza kuvifanyia kazi mdogo mdogo naamini nyakati zitaongea, kubwa zaidi kujifunza lugha mbalimbali ni muhimu ili tukiimba nyimbo zetu tuchanganye ili kuyafikia mataifa mbalimbali," anasema.

PHIN 02

ALICHOAMBIWA NA RUDALA

Anasema baada ya kuimba kava ya wimbo wa Rudala, alifanikiwa kukutana naye, kubwa zaidi alichojifunza utofauti wa kipindi chao na sasa na hekima, vitu alivyokiri vimempa nguvu mpya ya kupambana.

"Kwanza nimpe maua yake kwa sababu ya zawadi ya wimbo wa Nimekuchagua Wewe ambao kila unapopigwa unaonekana mpya, utaendelea kuishi miaka na miaka," anasema Phina na kuongeza:

"Alinishauri vitu vingi kuhusiana na muziki,uzoefu wake kabla na sasa vitu vinavyonipa mwanga, kubwa zaidi ni hekima iliyobeba mambo mengi ikiwemo na heshima aliyonayo ndani na nje."


SIRI YA UREMBO

Anasema anazingatia vyakula hasa vyenye tija na afya yake,anafanya mazoezi, anapumzika kwa wakati, anapenda kujifunza vitu vingi vinavyohusiana na urembo.

"Najitahidi kwa kiasi chake kuhakikisha nakula vyakula vitakavyolinda muonekano wangu, kwa sababu napenda fasheni tangu nikiwa mtoto kujua nivae vipi ili niweze kupendeza pamoja na kufanya dayati," anasema Phina na kuongeza;

"Kwangu muziki, fasheni na maisha ya kawaida vinakwenda kwa pamoja kwa asilimia kubwa najisimamia mwenyewe, inagwa kuna baadhi ya matukio nikialikwa nawashirikisha wabunifu wa mitindo ili kunishauri nivaaje."

PHIN 03

THAMANI YA MSICHANA

Anasema jambo la msingi ni upambanaji,kujitambua, ujasiri, namna ya kutumia kinywa, ulaji wenye staa mbele za watu, utembeaji na muonekano.

"Kitu kikubwa ni kujiamini, ndipo wasichana wanaweza wakatimiza ndoto zao, nje na hapo kila kitu watakachofanya wakikatishwa tamaa kidogo watajiona hawastahili," anasema Phina anayekiri kolabo zote alizowahi kufanya na wasanii mbalimbali zimemuongezea kitu katika muziki anaoufanya.


MEZA YA VIPODOZI (DRESSING TABLE)

Ingawa hajajua gharama sahihi ya kila mwezi inayoweza ikagharimu vipodozi vya kujaa katika meza (dressing table), anaeleza vitu muhimu visivyokosekana.

"Kwa sababu napenda muonekano mzuri na wa kuvutia muda wote, hapawezi kukosekana mekapu napenda brandi ya Rihanna pamoja na vitu vyote vinavyohusu usoni kwa  mtu anayezijua bei anaweza akazielewa, unyunyu (perfume) napenda kutumia za Sauvage Dior, hivyo siwezi kusema meza yangu ya vipodozi ni kiasi gani inagharimu kwa mwezi," anasema.

PHIN 04

NJE NA MUZIKI

Anasema kuhusu mpira wa miguu siyo mfuatiliaji ingawa anauelewa nao kidogo, hivyo hawezi kusema ni shabiki wa timu gani, lakini michezo anayoipenda ni gofu na tennis:"Hiyo ndiyo michezo inayonishawishi nikae chini na kuanza kuifuatilia nje na muziki."


UPO NYONYO

"Wimbo uliyonitambilisha Tanzania na Afrika Mashariki na Kati ni Upo Nyonyo baadaye zikafuatia Sisi Ni Wale,Manu ft Jay Melody na nyingine nyingi, ninachoshukuru nimefanikiwa kwa uharaka sijasota kama inavyowatokea baadhi ya wanii wenzangu," anasema.

Katika uandishi wake anasema anaanza na biti, akaiisikiliza inategemeana na siku inaweza ikamjia mistari ya mapenzi ama idea mbalimbali.

Kitu kinachomfurahisha ni ushindani uliyopo kwa wanamuziki wa kike nchini, anaona ni ishara ya kuonyesha muziki unakua lakini anaamini kila mtu ana njia yake ya kutoboa kimuziki.

"Keki ya mafanikio ni kubwa kila mtu ana njia inayoweza ikamtambulisha ndani na nje, hivyo ninapoona tupo wengi tunapambana inafurahisha na tunapaswa kufanya kazi kwa bidii ili Tanzania tukashindane levo za kimataifa," anasema.

Ukimuuliza ni sifa zipi za produzya anayependa kufanya naye kazi zake? Anajibu: "Hilo linategemea na pasheni yake, ubunifu ambao utafanya muziki uwe na mvuto na mzuri zaidi. Hivyo ndivyo vitu vya msingi navyovizingatia."

PHIN 05

CHANGAMOTO

"Nakutana na changamoto nyingi siwezi kutaja moja baada ya nyingine,kuna wakati unafanya nyimbo sokoni zinakuwa hazifanyi vizuri, lakini sikati tamaa nakuwa na mwendelezo na kuendelea kuwekeza pesa nikiamini ipo siku nitakula matunda yake," anasema Phina na kuongeza:

"Pia namna ya kufanya kazi na mameneja na maproduza, wadau wa muziki, Vyombo vya Habari,kila eneo lina changamoto zake, ila siyo vitu vinavyoweza kuzima ndoto zangu nitaendelea kupambana."

Anasisitiza kiwango cha muziki kinakuwa, lakini anaendelea kujifunza jinsi ya kuendana na soko la kimataifa,ambapo kitu kikubwa alichojifunza ni uwekezaji mkubwa unaofanyika na hilo ameanza kulifanyia kazi.

"Kwa Tanzania bado tunapaswa kujifunza uwekezaji mkubwa, ili tuingie katika levo ya ushindani wa kimataifa, pia kuna vikwazo vya lugha kwa maana ya kuchanganya lugha ili kuyafikia mataifa mbalimbali ingawa lazima tuzingatie Kiswahili."