Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eve Godwin atwaa taji la Miss Africa International 2026

Muktasari:

  • Eve alifanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupenya hatua mbalimbali za mashindano hayo hadi kufanikiwa kuingia sita bora (Top 6), kabla ya kutangazwa mshindi na kulitwaa taji hilo.

MREMBO kutoka Tanzania, Eva Godwin, ameandika historia baada ya kutwaa taji la Miss Africa International 2026, katika mashindano yaliyofanyika nchini Nigeria na kushirikisha warembo kutoka mataifa mbalimbali.

Eve alifanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupenya hatua mbalimbali za mashindano hayo hadi kufanikiwa kuingia sita bora (Top 6), kabla ya kutangazwa mshindi na kulitwaa taji hilo.

Ushindi huo umekuwa fahari kwa Tanzania, huku ukiweka alama nyingine katika safari ya mrembo huyo aliyeanzia kwenye mashindano ya ndani kabla ya kufanikiwa kufika kwenye jukwaa la kimataifa.

Miss Africa International yalianzishwa mwaka 2022, yakiwa na lengo la kutangaza utamaduni wa Afrika, kukuza utalii na ujasiriamali miongoni mwa wanawake vijana wa Kiafrika, pamoja na kuwapa jukwaa la kuhamasisha mabadiliko chanya katika jamii.


SAFARI YAKE ILIANZIA MISS GRAND TANZANIA

Safari ya Eva kuelekea kwenye mafanikio hayo ilianzia katika mashindano ya Miss Grand Tanzania 2026, ambayo fainali zake zilifanyika Agosti 8, 2026, jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo, Jihan ndiye aliyeibuka mshindi na kutwaa taji la Miss Grand Tanzania 2026, huku Eva akipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Africa International 2026.

Mashindano hayo yaliwakutanisha warembo kutoka maeneo mbalimbali nchini, yakitoa fursa kwa washiriki kujitokeza na kuwania nafasi za kuiwakilisha Tanzania katika majukwaa ya kimataifa.


AINGIA SITA BORA NA KUTWAA TAJI

Oktoba 22, 2026, Eva alianza safari ya kuelekea nchini Nigeria kushiriki mashindano ya Miss Africa International 2026.

Katika hatua za mwisho za mashindano hayo, Eva alifanikiwa kuingia kwenye orodha ya washiriki sita bora, akichuana na warembo kutoka Kenya, Denmark, Uingereza, Madagascar na Nigeria.

Kufuzu hatua hiyo kulimuweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania taji hilo, huku akionesha uwezo wa kushindana na warembo kutoka mataifa mbalimbali.

Safari ya Eve nchini Nigeria ilihitimishwa kwa mafanikio baada ya kutangazwa mshindi na kutawazwa Miss Africa International 2026.

Mafanikio yake yamepokewa kwa furaha na pongezi kutoka kwa wadau wa urembo, ambao wameendelea kumpongeza kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Kutwaa taji hilo ni hatua kubwa katika safari yake ya ulimbwende, ambayo imeanzia kwenye mashindano ya ndani na kumfikisha kwenye jukwaa la kimataifa.

Mbali na kuwa mafanikio binafsi, ushindi huo unaendelea kuonyesha nafasi ya mashindano ya urembo katika kukuza vipaji, kujenga uwezo na kutoa fursa kwa warembo wa Kitanzania kujitangaza nje ya mipaka ya nchi.

Taji la Miss Africa International 2026 linaongeza ukurasa mwingine wa mafanikio katika historia ya Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya kimataifa, likiungana na mafanikio ya Jihan Dimack aliyetwaa taji la Miss Grand International 2026, na kuifanya Tanzania kuendelea kujivunia ushindi katika majukwaa makubwa ya ulimbwende duniani.