Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda awakingia kifua watayarishaji wa maudhui mtandaoni

MAUDHUI Pict

Muktasari:

  • Aidha, Makonda amewataka wasanii mbalimbali kuendelea kuchukua fursa za kuchangamkia Sh2 bilioni ambazo zimetolewa kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wasanii kutokana na kazi zao.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewapongeza watengenezaji wa maudhui mtandaoni (Content Creator), kwa kazi kubwa ya wanayoendelea kuifanya ya kuitangaza nchi nje ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini, Dar es Salaam, Makonda amesema licha ya changamoto kubwa kwa baadhi ya watengeneza maudhui, ila wengi wao wanafanya vizuri jambo linaloonyesha umuhimu wa taifa letu.

"Niwapongeze sana kwa kazi kubwa wanaofanya, siwezi kuwahukumu nikiona mmaenda tofauti, kwa sababu unaweza ukawa na watoto saba ila mmoja wenu akaenda kinyume tu, hadi wenyewe mkajiuliza huyu kweli anatoka familia hii," amesema Makonda.

Aidha, Makonda amewataka wasanii mbalimbali kuendelea kuchukua fursa za kuchangamkia Sh2 bilioni ambazo zimetolewa kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wasanii kutokana na kazi zao.