Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lamata: Miss Tanzania 2026 itakuwa bab’kubwa

MISS Pict

Muktasari:

  • Safari hiyo inaendelea chini ya uongozi wa Leah Mwendamseke maarufu kama Lamata, ambaye alikabidhiwa usimamizi wa mashindano hayo Aprili 14, 2026, kutoka kwa Basila Mwanukuzi.

MISS TANZANIA 2026 inazidi kupamba moto, huku mwitikio mkubwa wa mashabiki na maandalizi ya kuvutia katika kanda mbalimbali vikiongeza ushindani na kurejesha mvuto wa mashindano hayo tofauti na baadhi ya misimu iliyopita.

Safari hiyo inaendelea chini ya uongozi wa Leah Mwendamseke maarufu kama Lamata, ambaye alikabidhiwa usimamizi wa mashindano hayo Aprili 14, 2026, kutoka kwa Basila Mwanukuzi.

Basila alikuwa akisimamia Miss Tanzania tangu mwaka 2018, baada ya kukabidhiwa jukumu hilo na marehemu Hashim Lundenga aliyekuwa akisimamia mashindano hayo tangu mwaka 1994.

Chini ya uongozi mpya, Miss Tanzania 2026 ilizinduliwa rasmi Septemba 10, jijini Dar es Salaam, ikiwa na kaulimbiu ya ‘Beauty for Positive Change’, inayolenga kuunganisha urembo na maendeleo ya kijamii, uongozi, utamaduni na uwezeshaji wa wanawake.

Akizungumzia mwenendo wa mashindano hayo hadi sasa, Lamata amesema anafurahishwa na namna Watanzania walivyoupokea mchakato huo, akimshukuru Mungu na kuwapongeza wananchi kwa kuonyesha uelewa na ushiriki mkubwa.


MIS 02

MWAKA HUU NI TOFAUTI

Akizungumzia tofauti ya mashindano ya mwaka huu na yaliyopita, amesema hatua za kanda zimekuwa na ushindani na maandalizi makubwa yaliyoongeza mvuto wa mashindano hayo.

“Tofauti ya Miss Tanzania zilizopita na hii ni kwamba kuanzia kwenye kanda, washiriki na wasanii wamefanya shoo nzuri na zimekuwa kubwa sana, yaani nadhani hii ndiyo Miss Tanzania yenyewe,” amesema Lamata.


MIS 04

KANDA TATU FRESHI

Mchakato wa mwaka huu unahusisha kanda saba ambazo ni Kaskazini, Kusini, Mashariki, Kati, Ziwa, Dar es Salaam pamoja na vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu. Hadi sasa, kanda tatu ambazo ni Kaskazini, Ziwa, na Kusini zimekamilisha usaili na hatua zake za kutafuta wawakilishi wa kuelekea mashindano ya kitaifa.

Kwa upande wa Kanda ya Kati, inayohusisha Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma itafanyika Oktoba 31, 2026.


MIS 07

SAPRAIZI ZA KUTOSHA KANDA YA KATI

Akizungumzia maandalizi ya kanda hiyo Lamata amesema wamejipanga kuleta vitu vya tofauti vitakavyowashangaza mashabiki na kuongeza ladha ya mashindano hayo.

Ameongeza kuwa washiriki pamoja na timu ya maandalizi wamejiandaa kuhakikisha wanaweka viwango vikubwa zaidi katika hatua hiyo.

Mbali na ushindani wa urembo, burudani pia inatarajiwa kuwa sehemu ya kivutio cha tukio hilo, ambapo wasanii Nandy, Gnako, Darassa na Stamina wanatarajiwa kutumbuiza, huku Heroes Band ikitarajiwa kuongeza ladha ya burudani kwa mashabiki watakaohudhuria.


MIS 03

CHANGAMOTO NA UZOEFU KWA LAMATA

Kuhusu changamoto anazokutana nazo katika kuendesha mashindano hayo, Lamata amesema zipo nyingi, hasa kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kubeba jukumu la kuandaa mashindano makubwa ya kitaifa kwa kiwango hicho.

Hata hivyo, amesema changamoto hizo zimekuwa sehemu ya kujifunza na kujenga uzoefu mpya katika tasnia ya mashindano ya urembo.

“Kwenye uandaaji kuna vitu vingi vya kujifunza moja baada ya lingine, lakini kwenye tukio lenyewe mambo yanaenda vizuri sana na tumeanza kwa ukubwa si haba,” amesema Lamata.


MIS 05

LAMATA AJIBU DAI LA MISS KUKOSA MVUTO

Kuhusu baadhi ya mashabiki wanaodai kuwa Miss Tanzania ya sasa haipati msisimko na umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, Lamata alipinga hoja hizo akieleza kuwa tangu alipotangazwa kukabidhiwa jukumu la kuendesha mashindano hayo, taarifa hiyo ilizungumzwa kwa kiwango kikubwa nchi nzima.

Amesema hata wakati wa uzinduzi wa mashindano na kutangazwa kwa maombi ya Miss Tanzania Open, kurasa mbalimbali kubwa za mitandao ya kijamii zilisambaza taarifa hizo.

“Mimi naomba wasubiri waendele kufatilia hadi fainali ya Miss Tanzania ndiyo watasema neno lolote Kwa sasa hivi ni mwanzo, siwezi kusema mengi ila Miss Tanzania mwaka huu ni kubwa watajionea wenyewe,” amesema Lamata.


MIS 06

WASHIRIKI 21 FAINALI

Katika msimu huu, waandaaji wamepanga kupata washiriki 21 watakaofika hatua ya fainali ya kitaifa, huku safari yao ikiambatana na mafunzo ya uongozi, ziara za kiutamaduni, mafunzo ya mawasiliano na shughuli za kijamii.

Pia mashindano hayo yanatarajiwa kuonyesha kupitia vipindi 34 vitakavyoonyesha safari za washiriki, utamaduni, mitindo na vivutio vya maeneo wanayotoka.


MIS 01

DESEMBA 12 KILELE  MISS TANZANIA

Fainali ya Miss Tanzania 2026 imepangwa kufanyika Desemba 12, jijini Dar es Salaam, huku waandaaji wakilenga kulifanya taji hilo kuwa zaidi ya ushindani wa urembo.

Lamata aliwaomba Watanzania kuendelea kuunga mkono mashindano hayo, akiahidi mabadiliko makubwa, burudani na uzoefu mpya katika safari ya kumpata mrembo atakayeshika taji hilo.

Amesema dhamira yao ni kuhakikisha Miss Tanzania inarejea kwa nguvu, inakuwa na mvuto mkubwa na kutoa jukwaa lenye thamani kwa washiriki wake.