Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jihan apenya Miss Grand International 2026

JIHAN Pict

Muktasari:

  • Fainali hiyo inatarajiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za Thailand, sawa na saa 7 mchana kwa Tanzania, huku maandalizi ya mwisho yakiwa yamekamilika baada ya hatua ya vazi la taifa iliyofanyika Oktoba 7, 2026.

KESHOKUTWA Oktoba 10, 2026 ni siku inayosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, baada ya Jihan Dimack kuifikisha nchi kwenye hatua ya mwisho ya Country’s Power of the Year ‘Nguvu ya nguvu ya mwaka’ na mashabiki wanampitisha kwa kuupenda ukurasa na kutoa maoni kwa wingi.

Sasa macho yanaelekezwa kwenye fainali ya Miss Grand International 2026, itakayofanyika Bangkok, Thailand. Jihan anayeipeperusha Bendera ya Tanzania, ameingia fainali ya pili ya kipengele hicho pamoja na Shyare Andrade wa Ecuador na mshindi anapata nafasi ya moja kwa moja kutinga 20 bora ya mashindano hayo.

Katika raundi hii ya mwisho, nguvu ipo pia kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki wanatakiwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kupitia chapisho rasmi la Jihan.

Kupenda ‘Like’ moja huhesabiwa kama pointi moja, kutoa maoni ‘Comment’ moja pointi moja, huku kuutuma tena ‘Repost’ ikiwa na pointi mbili, hivyo kila ushiriki unaweza kuongeza nguvu kwa Tanzania dhidi ya Ecuador.

Kesho pia ndiyo siku mashindano hayo mashindano hayo yanafikia kilele chake katika fainali itakayofanyika katika Ukumbi wa  MGI Hall, Bangkok na zaidi ya warembo 70 kutoka mataifa mbalimbali wanashindania taji linaloshikiliwa na Emma Tiglao wa Ufilipino.

Fainali hiyo inatarajiwa kuanza saa moja usiku kwa saa za Thailand, sawa na saa 7 mchana kwa Tanzania, huku maandalizi ya mwisho yakiwa yamekamilika baada ya hatua ya vazi la taifa iliyofanyika Oktoba 7, 2026.