Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diddy aumia kichwani adaiwa kupigana gerezani

DIDY Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Marekani, Combs, mwenye umri wa miaka 56, alikimbizwa hospitalini alfajiri ya Jumamosi baada ya tukio hilo linalodaiwa kutokea katika gereza la shirikisho la Fort Dix, New Jersey.

NEW YORK, MAREKANI: MSANII wa muziki wa hip-hop, Sean “Diddy” Combs, ameripotiwa kupata jeraha kubwa kichwani baada ya kudaiwa kupigana na mfungwa mwenzake mwenye asili ya Jamaica, Christopher Coke, anayejulikana kwa jina la “Dudus”.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Marekani, Combs, mwenye umri wa miaka 56, alikimbizwa hospitalini alfajiri ya Jumamosi baada ya tukio hilo linalodaiwa kutokea katika gereza la shirikisho la Fort Dix, New Jersey.

Awali, gazeti la Page Six liliripoti kuwa msanii huyo alipata tatizo la kiafya baada ya kugonga kichwa chake kwenye kitanda cha ghorofa gerezani. Hata hivyo, taarifa mpya za TMZ zilidai kuwa jeraha hilo lilitokana na ugomvi kati yake na Coke Ijumaa iliyotangulia.

DID 01

Vyanzo vilivyonukuliwa na chombo hicho vilidai kuwa Coke ndiye aliyekuwa na nguvu zaidi katika mapambano hayo, huku Combs akipata jeraha lililohitaji matibabu.

Taarifa hizo pia zilidai kuwa ugomvi huo ulichochewa na hasira za wafungwa wengine baada ya ripoti ya NBC News kufichua madai kuhusu maisha ya kifahari ya Combs gerezani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Combs alidaiwa kuwa na simu ya mkononi na pombe, pamoja na kuwanunulia wafungwa wengine dawa zinazotolewa kwa agizo la daktari.

Baada ya taarifa hizo kuvuja, maafisa wa gereza walifanya misako miwili na kukamata simu za mkononi zilizokuwa mikononi mwa baadhi ya wafungwa, akiwamo Coke.

DID 03

Coke, ambaye vyanzo hivyo vimemtaja kuwa na ushawishi mkubwa gerezani, anatumikia kifungo cha miaka 23 tangu mwaka 2012, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Combs aliripotiwa kuwa na fahamu na kuweza kuzungumza baada ya tukio hilo. Inadaiwa alirejeshwa gerezani kabla ya jua kuchomoza siku hiyo hiyo.

Baada ya ugomvi huo, Combs na Coke walidaiwa kuwekwa katika vyumba vya kutengwa kwa muda wa wiki mbili kama adhabu.

Msemaji wa Combs alikuwa ameiambia Page Six kuwa timu yake ilikuwa inafuatilia taarifa hizo ili kuthibitisha mazingira halisi ya tukio hilo.

“Afya na ustawi wa Sean ni jambo letu la kipaumbele kwa sasa,” amesema msemaji huyo, akiwashukuru watu walioonyesha kujali hali ya msanii huyo.

DID 02

Combs alihukumiwa kifungo cha miezi 50 katika gereza la Fort Dix mwaka uliopita baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili yanayohusiana na ukahaba. Hata hivyo, aliachiwa huru dhidi ya mashtaka mazito zaidi ya kuendesha mtandao wa uhalifu na biashara ya usafirishaji wa watu kwa madhumuni ya ngono.

Hii si mara ya kwanza kwa Combs kuripotiwa kuhusika katika tukio la ugomvi gerezani. Mwezi Julai, alidaiwa kupelekwa katika chumba cha kutengwa baada ya kutokea kwa mapambano na mfungwa mwenzake.

Pia, muda wake wa kukaa gerezani uliripotiwa kupunguzwa tena mwezi Septemba. Awali, aliazimwa kuachiliwa Mei 8, 2028, lakini tarehe hiyo ilihamishwa hadi Januari 21, 2028.