Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Billnass amvisha pete ya uchumba Nandy

Muktasari:

Msanii wa muziki nchini Tanzania,  Billnass  amemvalisha pete ya uchumba msanii mwenzake, Faustina Charles maarufu Nandy.

Dar es Salaam. Msanii wa muziki nchini Tanzania,  Billnass  amemvalisha pete ya uchumba msanii mwenzake, Faustina Charles maarufu Nandy.
Siku za hivi karibuni wawili hao wamekuwa karibu na kushirikiana katika masuala mbalimbali na haikuwa ajabu walipotoa wimbo wa pamoja unaoitwa Bugana.
Jana usiku Ijumaa Aprili 10, 2020 Billnass alimvalisha pete Nandy aliyekuwa katika kipindi kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja mtandaoni na televisheni ya TVE.
Billnass akiwa amevaa koti jeusi na suruali nyeupe alimvisha pete mkali huyo wa wimbo Ninogeshe wakati akiimba wimbo wake wa Labda nizikwe.
Kabla ya kumvalisha pete, alipiga magoti huku Nandy akionekana kutoamini kilichokuwa kikiendelea, alianza kutokwa machozi huku akiwa ameshikilia kipaza sauti.
Billnass ambaye jina lake halisi ni William Lyimo akiwa mbele ya Nandy amesema, “leo ni siku yangu ya kuzaliwa naamini tumekuwa  pamoja muda mrefu, tumepitia vitu vingi vizuri na vibaya najua upande wako mzuri na upande wako mbaya nimechagua vyote, natamani dunia nzima ijue nakupenda, nakupenda.”
"Katika maisha yangu sijawahi kufanya kitu kikubwa kama hiki kwa hiyo leo ni siku muhimu sana ni siku ya kipekee. Naamini ndio mwanzo wa ukurasa mwingine wa maisha yangu kwa hiyo ambacho naweza kukuambia nazidi kukuombea usiwe mzuri tu kwangu bali kwa mama na watoto wangu.”