Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Andrew Sekedia afariki dunia, dada yake ataja chanzo cha kifo

KIFO Pict

Muktasari:

  • Kifo chake kinaacha pengo kwa wadau wa muziki wa dansi, ambao wamekuwa wakitambua mchango wake kupitia safari yake ya muziki na uwezo wake wa kupiga kinanda katika bendi alizowahi kushiriki.

Muziki wa dansi nchini umepata pigo baada ya mwanamuziki nguli, Andrew Sekedia, aliyefahamika kwa umahiri wake wa kupiga kinanda, kufariki dunia leo Novemba 27, 2026, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, dada wa marehemu, Betty Sekedia, amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo, ambalo awali hakuwa akilitambua na kudhani anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

“Tatizo la moyo lilikuwepo, ila alikuwa hajajua, alikuwa anajua bado ni vidonda vya tumbo,” amesema Betty.

Betty amesema ndugu yao alianza kupata matibabu wiki hii, akieleza kuwa Jumatatu alianza kliniki katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), lakini jana hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuwalazimu kumpeleka hospitalini kwa matibabu zaidi.

KIF 01

Amesema awali walimpeleka kwenye zahanati kabla ya kuhamishiwa hospitali, ambako walifika majira ya saa tano usiku na kuendelea na vipimo hadi asubuhi.

“Jana Novemba 26, 2026 ndiyo akazidiwa, hali ikamshika. Tulianza pale dispensary, baadae akahamishiwa Muhimbili . Vipimo vilifanyika mpaka asubuhi, baadaye tukahamishiwa Jakaya, akapewa kitanda, lakini hata nusu saa haijamaliza ndipo akafariki,” amesema Betty.

Sekedia alikuwa mwanamuziki mwenye uzoefu mkubwa katika muziki wa dansi, akijulikana zaidi kwa umahiri wake wa kupiga kinanda, chombo kilichomfanya kuwa sehemu muhimu ya bendi mbalimbali alizowahi kufanya nazo kazi.

KIF 03

Katika safari yake ya muziki, amewahi kupita katika bendi za Akudo Impact, Malaika Band, Town Classic, Musica, Diamond Sound na African Revolution, maarufu Tam Tam, pamoja na nyingine nyingi.

Kifo chake kinaacha pengo kwa wadau wa muziki wa dansi, ambao wamekuwa wakitambua mchango wake kupitia safari yake ya muziki na uwezo wake wa kupiga kinanda katika bendi alizowahi kushiriki.