Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Akili, utimamu vilivyowabeba Simba

Muktasari:

  • Kama ulitazama vyema mechi ya Jumamosi, kuna mambo makubwa mawili muhimu ambayo ni akili na utimamu wa mwili wa mchezaji mmoja mmoja ndio mpango mzima wa klabu za kufanikiwa. Katika mechi ya watani maarufu kama Kariokoo Derby, ufundi ulionyeshwa na mshambuliaji Mpanzu  ambaye alitoa mchango katika ushindi huo na kufunga goli la ushindi katika kipindi cha pili.

JUMAMOSI iliyopita ilikuwa siku ya mechi kali za kusisimua ikiwamo ya watani wa jadi Simba na Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru maarufu kama Shamba la Bibi jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliojaa ufundi mwingi, siku hiyo Simba ndio walikuwa bora ziadi katika kila eneo ikiwamo utimamu wa kiafya na kufanikiwa kuibamiza Yanga bao 2-1.

Kama ulitazama vyema mechi ya Jumamosi, kuna mambo makubwa mawili muhimu ambayo ni akili na utimamu wa mwili wa mchezaji mmoja mmoja ndio mpango mzima wa klabu za kufanikiwa. Katika mechi ya watani maarufu kama Kariokoo Derby, ufundi ulionyeshwa na mshambuliaji Mpanzu  ambaye alitoa mchango katika ushindi huo na kufunga goli la ushindi katika kipindi cha pili.

Kwa jicho la kitabibu, haikuwa pekee utimamu wa mwili wa mchezaji bali pia kucheza kwa kutumia akili tulivu hasa kwa wachezaji wa eneo la kiungo Simba waliweza kuwaweka kapuni Yanga na kumiliki mpira kwa zaidi ya asilimia 60.

Mbinu waliyotumia Simba kwa kuweka kambi nchini Afrika kwa wiki kadhaa ni moja ya mbinu bora kwa ajili ya maandalizi ya kisaikolojia na ya kimwili. Mazingira ya huko yalikuwa ni ya kuwapa utulivu kiakili hatimaye kushikamana na maelekezo ya Kocha wao.

Mchezaji anapocheza kwa kutumia akili na kufanya uamuzi sahihi, ni lazima awe utulivu mzuri kihisia ikiwamo kutokuwa na woga, hofu au msongo wa mawazo. Katika bao la pili Mpanzu alimalizia vyema pasi ndefu na kuweza kunyumbulika na kuwahadaa mabeki na kipa bora wa Yanga, utulivu na kujiamini kwake ndiko kulimbeba sana wakati akifunga.

Kawaida mchezaji akiwa na hofu au woga ni vigumu kuweza kufanya maamuzi sahihi ya kiakili ili kukupa matokeo mazuri uwanjani.

Huitaji ustahimilivu wa kihisia wakati wa nyakati za mashinikizo ya uwanjani ikiwamo kulaumiwa na mashabiki pale wanapokosea. Wote tunafahamu mechi za watani zilivyo na lawama na shinikizo kubwa. Kwa upande mwingine wachezaji wanapocheza uwanjani wanahitaji sana kupata hamasa toka kwa mashabiki ili kuwatuliza kiakili. Vile vile wanahitaji maandalizi ya kiakili kupitia bench la ufundi lenye wataalam wa saikolojia kuweza kukabiliana na matatizo ya kiakili kwenye mechi za ushindani.

Kwa upande wa Simba walikuwa kama vile wameishapoteza, hii ni baada ya kufungwa bado dakika ya 5 ya mchezo na huku Ikizingatiwa hawajaifunga Yanga tangu 2023. Lakini baadaye wachezaji wa Simba walituliza akili, wakaweka woga wa kupoteza pembeni na hatimaye waliweza kurudisha bao na kufunga la ushindi lililoamsha furaha kubwa kwa wana Msimbazi. Mechi hizi zilionyesha kuwa akili na utimamu wa wachezaji ndio mpango mzima ili kuweza kupata matokeo makubwa katika mechi zenye ushindani.

Unaweza kuwa na wachezaji wenye utimamu wa mwili asilimia 90, lakini mchezaji akikosa utulivu wa akili huwa ni ngumu kupata matokeo.

Akili ya mchezaji yenye utilivu ndio inayopokea maelekezo ya kocha haraka na kwa usahihi, hatimaye kwenda kubadili mbinu ili kupata matokeo mazuri. Akili ya mchezaji inahitaji kuwa katika hali bora kiafya ili kupokea, kuweka kumbukumbu, kufikiri na kutafsiri mapokeo na kufanya uamuzi sahihi. Soka la kisasa limejaa ufundi mwingi, kila wakati wachezaji hupewa maelekezo mapya kwa maneno na ishara ili kuendana na hali ya mchezo.


Kinachovuruga akili ya mchezaji

Woga wakuwa mkosaji ni tatizo ambalo linawasumbua sana wachezaji wa soka, hasa wanapokaribia kupata mafanikio. Mfano wachezaji wa Yanga wao ni bora kwa muda mrefu mbele ya Simba, kuwa na hofu ya kupoteza ni kawaida.

Mara kwa mara woga kabla ya mechi hujitokeza, lakini uzoefu na ustahimilivu huweza kuwasaidia kujiamini na kupata utulivu wa kiakili dimbani.

Ni kawaida mashabiki na kuvurugwa na kushindwa kuwahamasisha wachezaji, huwa wanachotaka ni kushindwa tu na si vinginenevyo.

Huwa ni kawaida mashabiki ambao timu yao iliyotoka kufanya vibaya kutoshabikia kwa nguvu, hii ni kutokana na kuathirika kisaikolojia.

Wachezaji wasiposhangiliwa ili kuwapa hamasa hujikuta akili zao zinaathirika na kukosa utulivu, hii huwafanya kukosea kizembe uwanjani.

Suala la mikataba na malipo, mchezaji akikosa stahiki zake huwa na hisia hasi ikiwamo hasira au msongo wa mawazo na pia kukosa hamasa.

Hali ambayo humpa shinikizo la akili, hatimaye kushusha utendaji wa kiakili. Hata kama yuko timamu kimwili huweza kucheza chini ya kiwango.

Mchoko wa mwili na akili, mchezaji anayetumika sana bila kupumzishwa hukabiliwa na uchovu sugu ambao unaweza kumfanya kucheza akiwa na maumivu ya mwili. Hali hii inachangia akili yake kushindwa kuzingatia majukumu vizuri anapokuwepo uwanjani.

Vile vile uchovu wa akili unaweza kumkabili mchezaji endapo ana msongo wa muda mrefu wa mawazo au anapokosa mapumziko.

Na pia anaweza kuwa na uchovu wa akili kutokana na akili yake kukosa muda wa kuburudika, kupumzika na kulala vizuri.

Kukosa kujiamini kwa mchezaji kunaweza kuchangiwa na hali ya kupata mafunzo chini ya kiwango na pia kuwa majeruhi mara kwa mara.

Shinikizo la ndani na nje ya uwanja, hii inaweza kumpa hofu na uwoga hatimaye kukosa utulivu wa akili na kushindwa kufanya mauamuzi sahihi.

Mara nyingi shinikizo kubwa ni kutoka kwa mashabiki, kocha na benchi la ufundi, wachezaji wenzake na vyombo vya habari.


Utimamu mwili uko hivi

Utimamu wa mwili kwa wachezaji wa mpira wa miguu inahitaji mbinu zilizowiana na pana pamoja na nguvu, kasi, wepesi, uvumilivu na umnyumbulikaji.

Hii ni kwasababu mpira wa miguu ni mchezo wa mgumu na muda mwingi kutumia nguvu nyingi. Wachezaji lazima wapewe mazoezi na mafunzo yenye kuzingatia weledi ili kukabiliana na dakika 90 za mchezo.

Mambo mengi ya ndani ya uwanja hujumuisha kubadilishana kati ya kukimbia, kutembea na kukimbia kwa kasi kwa kiwango cha juu. Bila hivyo ni vigumu mchezaji kucheza kwa kiwango na kwa akili.

Wanahitaji utimamu ili kustahimilivu na kuwa wakakamavu na hatimaye kudumu uwanjani muda mrefu bila kuchoka.

Mazoezi na mafunzo, lishe na mapumziko ni moja ya nyenzo ya msingi ili mchezaji kuwa na utimamu wa juu.

Chukua hii

Mchezaji mwenye utimamu wa juu anahitaji akili yenye utilivu, ndio maana pamoja na klabu za kisasa  licha ya kujenga vituo vya kisasa vya kuwafua wachezaji wao lakini pia wana wataalamu wa afya akili na wanasaikolojia.

Simba kujichimbia Afrika Kusini ni bonge moja la mbinu iliyowabeba kuweza kuwa bora katika mchezo huo hatimaye kucheza kwa kiwango cha juu mpaka katika mechi iliyofuata ya juzi walipoibamiza Mashujaa FC kwa mabao 6-1.