Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahera afurahia Yanga kucheza usiku

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya kwanza kwa Yanga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika itachezwa kwenye Uwanja wa Julai 5 jijini Algiers.

Algiers, Algeria. Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kitendo cha mchezo wao dhidi ya USM Alger kuchezwa nyakati za usiku ni faida kwa timu yake.

Mechi hiyo ya kwanza kwa Yanga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika itachezwa kwenye Uwanja wa Julai 5 jijini Algiers.

Zahera alisema mechi inapochezwa usiku inakuwa na faida kubwa kiufundi kulinganisha na mchana au jioni.

Alizitaja faida hizo kuwa ni wachezaji kutochoka haraka pamoja na mfumo mzuri wa upumuaji.

Kuhusu hali ya hewa ya baridi, Zahera alisema hana hofu nayo na hawezi kuifanya kama kisingizio