Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamtetea Yondani, Ajib

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema, wachezaji hao hawajasafiri si kukusudia, lakini kwa sababu ya matatizo hayo.

 Dar es Salaam. Uongozi wa Yanga umewakingia kifua wachezaji wake Kelvin Yondani 'Vidic', Ibrahim Ajib, Papy Tshishimbi na Mzambia Obrey Chirwa walishindwa kusafiri na timu kwenda nchini Algeria kwa sababu ya matatizo mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema, wachezaji hao hawajasafiri si kukusudia, lakini kwa sababu ya matatizo hayo.

Mkwasa alisema, Yondani na Tshishimbi wao walipata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, Obrey ana malaria wakati Ajib anamwangalia mke wake anayetarajiwa kujifungua hivi karibuni.

"Kama nilivyosema, Yondani, Tshishimbi na Chirwa wao ni wagonjwa na Ajib amebaki kwa sababu mkewe anakaribia kujifungua,"alisema Mkwasa.

Kikosi cha Yanga kilisafiri na Ndege ya Emirates jana Alhamisi kwenda Algeria wakipitia Dubai tayari kwa

mchezo huo utakaochezwa kesho kutwa Jumapili dhidi ya  USM Alger.

Wachezaji wa Yanga waliondoka na timu ni Rostand Youthe, Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Andrew Vincent, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Pato Ngonyani, Said Makapu,  Juma Abdul, Yussuf Mhilu, Mwashiuya Geoffrey, Pius Buswita, Rafael Daud, Yohana Nkomola, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi,  Abdallah Shaibu 'Ninja', na Said Makapu.