Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga: Nyie chongeni weee lakini mtatuelewa tu

Muktasari:

Mchezaji huyo amesisitiza kwamba wao wanajua wanachokifanya, lakini mwisho wa siku hao wapinzani wao walioanza kwa mikwara watanywea tu na Yanga itarudi kwenye nafasi yake ya ubingwa.

BEKI wa Yanga, Haji Mwinyi, amesema Ligi Kuu Bara ipo kwenye hatua ya  kupunguzana pointi na inatokana na wachezaji kuwa na hamu ya kujitengenezea ufalme mapema mbele ya mashabiki.

“Kipindi hiki ni cha wachezaji wapya kwa kila timu kuonyesha uwezo wao hadi tone la mwisho, hilo litawasaidia kuwajengea imani kwa mashabiki wao kwamba hawakukosea njia kuwasajili, hilo linapelekea kushindwa kuwa na uimara wa nani anaweza anamudu kukaa kileleni, lakini itafikia wakati wa kujua nani ni nani na nini kitakachovunwa kwa msimu huu,” alisema.

Mchezaji huyo amesisitiza kwamba wao wanajua wanachokifanya, lakini mwisho wa siku hao wapinzani wao walioanza kwa mikwara watanywea tu na Yanga itarudi kwenye nafasi yake ya ubingwa.

Kwa upande wake alisema anaanza  kupambana kurejesha heshima ya namba ndani ya kikosi cha kwanza cha  kocha Mzambia George Lwandamina na akifanikiwa hilo ndipo atajua afanye jipya gani ndani ya Yanga.

“Anayepata nafasi Yanga anafanya kweli, hii inatusaidia wachezaji kuwa makini uwanjani, naamini nitacheza kwani ligi bado ni mbichi, naendelea kujifunza mapungufu yangu na ubora wangu,” alisema.