VIDEO:Manara arusha kijembe Simba kufunika tuzo za Ligi Kuu

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kwamba timu hiyo imezifunika klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu ulioisha kwa kunyakua tuzo nyingi zilizotolewa jana Jumamosi usiku kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Manara alisema timu hiyo imejipanga vyema kwa ajili ya msimu ujao licha ya kuongezeka timu na kufikia 20.

Alisema kwamba suala la kuongezeka timu halimpi tatizo bali miundombinu kwa ujumla kwani itazilazimu timu kusafiri umbali mrefu zaidi.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara waliibuka na kitita cha Sh 96 milioni baada ya kufanikiwa kutwaa taji hilo.

Katika halfa ya utoaji wa tuzo hizo, Simba kilipenyeza wachezaji watano kwenye kikosi bora cha cha Ligi Kuu msimu ulioisha.

Wachezaji wanaounda kikosi bora cha Ligi Kuu 2017/2018
Aishi Manula
Hassan Kessy
Shaffiq Batambuze
Erasto Nyoni
Kelvin Yondani
Papy Tshishimbi
Shiza kichuya
Tafadzwa Kutinyu
Emmanuel Okwi
John Bocco
Marcel Boniventure