Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tegete aipa Yanga ubingwa mapemaa

“Yanga iko vizuri tu, nina imani kubwa itatetea ubingwa msimu huu kikubwa sasa ni kujipanga tu kwenye michuano ya kimataifa.”
– John Tegete - kocha mkongwe Tanzania

KOCHA Mkongwe nchini, John Tegete ameviangalia vikosi vya Simba na Yanga na kutoa tathmini yake kwamba hakuna namna wazee wa Jangwani watashindwa kuondoka na taji la Ligi Kuu msimu huu.

Tegete ambaye mwanaye Jerryson Tegete alicheza Yanga kwa mafanikio, alisema mashabiki wa timu hiyo waanze kuandaa shampeni kwa ajili ya kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Kocha huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, alisema Yanga wamekamilika idara zote ndani ya uwanja lakini wapinzani wao Simba ni wazuri katika kiungo na ushambuliaji lakini beki yao iko ovyo.

Tegete alisema kwake msimu huu anaipa nafasi kubwa Yanga ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu iwapo tu uongozi wa timu hiyo utaendelea kumwamini Kocha George Lwandamina.

“Timu iko vizuri tu nina imani kubwa watatetea ubingwa msimu huu kikubwa sasa ni kujipanga tu kwenye michuano ya kimataifa hivyo mashabiki wajiandae kushangilia taji hilo,” alisema.