Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msimbazi wapewa majina ya kusajili

Muktasari:

  • Mwameja, ambaye alikuwa kipa tegemeo klabuni hapo, amekiangalia kikosi hicho na kubaini kuwa licha ya uwepo wa James Kotei na Jonas Mkude ambao walibamba msimu uliopita, lakini bado anahitajika mtu mwenye utamu kama wa Mudathir Yahaya aliyetua Azam FC.

WAKATI harakati za usajili ndani ya Simba zikipamba moto, staa wa zamani wa kikosi hicho, Mohamed Mwameja, amewapa majina mawili tu ya wachezaji ambao wanatakiwa kusajiliwa maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Mwameja, ambaye alikuwa kipa tegemeo klabuni hapo, amekiangalia kikosi hicho na kubaini kuwa licha ya uwepo wa James Kotei na Jonas Mkude ambao walibamba msimu uliopita, lakini bado anahitajika mtu mwenye utamu kama wa Mudathir Yahaya aliyetua Azam FC.

“Kama wamechelewa kwa Mudathir basi waangalie kiungo mwingine wa staili hiyo, lakini wakiridhika kwa kuona safu imekamilika basi wawe makini kwa kuangalia mchezaji sahihi,” alisema Mwameja.

Lakini, kwa upande wa safu ya makipa, alisema licha ya Aishi Manula kucheza mechi 28, ni vigumu kupima uwezo wake kwa kuwa hakupata ushindani kutokana na Said Mohamed ‘Nduda’ kuwa majeruhi na Emmanuel Mseja kutokuwa kwenye kiwango cha kizuri.

“Manula ni mzuri, ila Simba inatakiwa kuwa na makipa watatu wakali ambao wana uwezo sawa wa kuanza kikosi cha kwanza, kama tulivyokuwa kipindi kile ambapo nilikuwa mimi, Idd Pazi na Makenzi Ramadhan, kocha alikuwa anaamua ampange nani hata ikitokea mmoja hayupo hakuna shaka,” alisema.

Alimtaja kipa wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinoco, kuwa ni aina ya kipa wanayestahili kuwa naye ndani ya kikosi hicho na kuweka wazi kwamba, mapungufu yake ni madogo na rahisi kuyarekebisha.

“Safu ya makipa ikiwa na Tinoco, Nduda na Manula, watakuwa na ushindani kama ilivyofanya Yanga kwa Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ ambao waliisaidia Yanga isifungwe kirahisi na walipoondoka tu hawakuwa na utulivu mzuri,” alisema.

Mwanaspoti lilimtafuta Tinocco kujua endapo Simba wakimpa ofa ya kukitumikia kikosi chao atakuwa tayari kuikubali.

Alijibu: “Kazi yangu ni kucheza, kikubwa ni wao kuzingatia sheria kwa kufanya mazungumzo na mabosi wangu hivyo popote kwangu kambi.”