Yanga yapewa ujumbe mzito!
Muktasari:
- Asisitiza kati ya Tambwe au Ngoma wangemuondoa mmoja ili watafute nafasi ya kuingiza mshambuliaji mmoja mwenye makali.
Kocha msomi zaidi nchini, Profesa Mshindo Msolla aliyewahi kuinoa Taifa Stars, amesisitiza kwamba Yanga ina upungufu na kabla ya haijaingia katika Ligi ya Mabingwa wanatakiwa kufumba macho na kuvunja benki kuingia sokoni kutafuta vifaa vya maana haswa kwenye fowadi.
"Yanga ina upungufu mwingi ambao ni lazima waufanyie kazi haraka kabla ya kuingia katika mashindano makubwa anza kuangalia safu yao ya ushambuliaji sasa wanategemea nguvu ya Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa wale Ngoma na Tambwe bado ni majeruhi,"alisema Msolla.
"Majeruhi ya Tambwe na Ngoma na hata yule Thabaan Kamusoko sio kitu kidogo kutokana na umri watakuwa wanahitaji muda mrefu zaidi lakini timu yao inaumia sasa mtazamo wangu ni kwamba kati ya Tambwe au Ngoma wangemuondoa mmoja ili watafute nafasi ya kuingiza mshambuliaji mmoja mwenye makali.