Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo chamtibua kocha Yanga, acharukia mabosi kuhusu usajili

Muktasari:

  • Yanga ilikumbana na dhahama hiyo katika mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kasarani, jijini Nairobi.

KIPIGO cha mabao 4-0 ambacho Yanga ilikumbana nacho juzi Jumatano usiku mbele ya Gor Mahia kule Kenya, kimemwachia mshituko mkubwa kocha Mwinyi Zahera na sasa Mkongomani huyo kasema lazima kikosi chake kisukwe upya.

Yanga ilikumbana na dhahama hiyo katika mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kasarani, jijini Nairobi.

Zahera ambaye hakukaa katika benchi la ufundi kutokana na kukosa kibali cha kazi, amebadili gia baada ya kuona viwango vya wachezaji wake na sasa anatakiwa kuifanyia mabadiliko makubwa timu hiyo.

“Hapana. Ni lazima tufanye kitu cha maana, ninapaswa kukutana na viongozi wa Kamati ya Usajili, kuna haja ya kukijenga kikosi upya,” alisema kocha huyo.

“Kwanza nataka wafanye haraka usajili wa wachezaji niliowapendekeza kulingana na maeneo husika, hii itasaidia kuirudisha timu katika hali yake. Pia wachezaji muhimu waliomaliza mikataba nao washughulikiwe, wana msaada mkubwa ndani ya timu, sitapenda kusikia wanaondoka.

“Mabadiliko ya timu hasa kwa wachezaji wapya ni muhimu, ni lazima kufanya hivyo haraka, ingawa hawatatumika katika mashindano haya.”

Alisema wamepoteza mechi ya Gor Mahia kwa sababu timu haikuwa pamoja kwa muda mrefu.

“Nitawaomba viongozi tusivunje kambi ili tukae pamoja kujenga timu na kurekebisha makosa yaliyojitokeza,” aliongeza Zahera.

AWATAKA HARAKA NGASSA, KASEKE

Kuonyesha namna alivyokerwa na kipigo hicho, Zahera kaagiza kuwa akifika Dar es Salaam anataka awakute mazoezi wachezaji wote wapya ili awe nao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ukaoanza mwezi ujao.

Zahera amekwenda mbali akiwaambia viongozi wake wafanye haraka na kuhakikisha kama inawezekana majina ya Mrisho Ngassa, Deus Kaseke na straika Mkongomani Bakambo, yafike haraka Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Katika usajili wa dirisha dogo wa CAF ambao Yanga walitakiwa kuongeza majina matatu, walichelewa kutuma majina hayo kwa sababu kuna mambo hawakukamilisha.

“Naomba viongozi wafanyie kazi hilo kwa haraka kwani tukiwatumia wachezaji hawa katika mechi ijayo na Gor Mahia itakuwa vizuri, wanaweza kuongeza kitu katika timu,” alisema.