Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera yamkingia kifua Maxime

Muktasari:

  • Maxime ni nahodha wa zamani wa Taifa Stars amekuwa na mafanikio tangu alipoanza kuchukua majukumu ya ukocha akiwa na Mtibwa Sugar na sasa Kagera Sugar

Dar es Salaam. UONGOZI wa Kagera Sugar umesema  haukatishwi tamaa na matokeo mabaya wanayopata katika mechi za Ligi Kuu huku wakiamini kwamba kocha wao bado ana nafasi ya kushika nafasi bora za juu.

Kagera Sugar ambayo msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu huku kocha wao Mecky Maxime akiwa kocha bora wa msimu, kwasasa anaburuza mkia katika msimamo.

Katibu mkuu wa klabu hiyo,  Salum Madaki alisema katika kipindi cha mpito hawakati tamaa kwani hata wachezaji wao wanne walikosekana kwenye mechi za awali wakiwa majeruhi wakiwemo Peter Mwalyanzi,  Mohamed Fhaki, George Kavila.

"Tunamwamini kocha wetu na wala hatuna hofu naye kwani tunaamini anapitia kipindi cha mpito kama ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu uliopita. Tunaamini ataendelea kuwa kocha bora na hatutamwingilia majukumu yake ya kazi kwasababu tu ya timu kupata matokeo mabaya.

"Kuna baadhi ya wachezaji hawakucheza mechi zilizopita japokuwa hawakuwa na majeruhi lakini huo ni mfumo wa kocha mwenyewe huwezi kumpangia kikosi tunachotaka ni kumwamini tu ili atupe matokeo mazuri,  mechi, zote tulizocheza zilikuwa ngumu mno kwetu, " alisema Madai.

Kagera Sugar wamecheza mechi tano ambapo mbili walikuwa nyumbani huku tatu wakiwa ugenini,  wana pointi mbili ambazo walizipata katika mechi zao mbili walizotoka sare.