Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Dilunga na Simba ipo hivi

Muktasari:

  • Kamati ya Usajili ya Simba inafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi ambalo liliomba kuongezewa nguvu kwa kufanyiwa usajili katika nafasi ya beki wa kati ambayo Pascal Wawa ameshamwaga wino.

KIUNGO fundi wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga, amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba inayotajwa kumhitaji kwa hali na mali ili kuongeza nguvu katika safu ya kiungo.

Kamati ya Usajili ya Simba inafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi ambalo liliomba kuongezewa nguvu kwa kufanyiwa usajili katika nafasi ya beki wa kati ambayo Pascal Wawa ameshamwaga wino.

Pengine ni eneo la ushambuliaji ambapo tayari wameshawanasa mastraika wanne huku eneo la kiungo ndio wanahangaika kumalizana na Dilunga ambaye ameshamalizana kila kitu na uongozi wa Simba.

Iko hivi, Dilunga amefanya mazungumzo na kamati ya usajili ya Simba na wameshamalizana huku akiwa ameshapewa mkataba kilichobaki ni kusaini.

Kinachokwamisha Dilunga ni Simba kutofikia makubaliano na Mkurugenzi wa Mtibwa, Jamal Byser.

“Kinachomkwamisha Bayser kuniachia ni kutokana ofa kutoka Difaa El Jadida (anayoichezea Simon Msuva), lakini wameonekana hawapo siriazi sana kama Simba,” alisema Dilunga.

“Binafsi nimeshaongea na Simba.”