Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Banka akitua tu, Makambo atamzidi Kagere

Mohammed Issa ‘Mo Banka’

Muktasari:

  • Viungo hao wenye uwezo wa kukaba na kupiga pasi za mabao kwa pamoja, huku Abdallah Shaibu ‘Ninja’ akicheza nyuma yao kwa lengo kuwapa uhuru na kumpigia pasi safi Makambo

KOMBINESHENI ya viungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Papy Tshishimbi, imekuwa tamu na kali ndani ya Ligi Kuu Bara kwa namna wanavyocheza, wakimrahisishia kazi straika Heritier Makambo ndani ya Yanga katika kutupia kambani.

Viungo hao wenye uwezo wa kukaba na kupiga pasi za mabao kwa pamoja, huku Abdallah Shaibu ‘Ninja’ akicheza nyuma yao kwa lengo kuwapa uhuru na kumpigia pasi safi Makambo.

Hata hivyo, Fei Toto amefunguka na kudai licha ya kuelewana na Tshishimbi, lakini siku akitua Mohammed Issa ‘Mo Banka’ basi Makambo atakuwa anafunga sana na ikiwezekana kumfunika kabisa straika wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao matatu katika Ligi Kuu kwa sasa.

“Yanga itakuwa haishikiki katika safu ya kiungo kama Mo Banka naye akifika mapema tutakuwa tunaupiga mwingi na pasi za kumwaga kwa Makambo, ili aifanye kazi yake ya kufunga kwa ufanisi,” alisema.

Aliongeza baada ya kucheza na Tshishimbi, amejikuta akijifunza vitu vingi ambavyo vitamsaidia katika uchezaji wake sasa na katika maisha yake ya soka kwa baadaye.